Na FC
BODI ya ukaguzi wa filamu na michezo ya kuigiza imeanza kuwashukia
wale wote wapenda kuvaa vimini na kushiriki katika filamu za
Swahiliwood, hayo yameongewa na katibu wa Bodi ya filamu nchini Bi.
Joyce Fisso baada hivi karibuni kukutana na mwigizaji na mtayarishaji wa
filamu Aunty Ezekiel.
Msanii huyo aliitwa na Bodi baada ya filamu hiyo kufika hapo kwa
ajili ya ukaguzi wa filamu hiyo na kukutana na jopo la wakaguzi
waliompata ushirikiano kwa kumshauri sehemu za kuzirekebisha bila
usumbufu, jambo lilomfurahisha Aunty Ezekiel.
.
“Nashukuru bodi wamekuwa waelewa ,wamenielekeza kurekebisha baadhi ya
vipengele ili kuboresha filamu yangu naahidi kuirekebisha kwani
vinarekebishika.”alisema Aunt Ezekiel.
Aidha Aunt Ezekiel ameomba radhi kwa kutopeleka script yake ya filamu
hiyo mpya ya SCOLA Bodi ya Filamu na amesema atakuwa akiwasilisha
miswada yake kabla ya kutengeneza filamu zake. Aidha amewahakikishia
watanzania kuwa atakuwa mfano bora katika kutengeza filamu bora na zenye
maadili.
Kwa upande wake Katibu Mtendaji wa Bodi hiyo Bi.Joyce Fissoo ameeleza
kuwa kuna umuhimu wa wasanii kufuata sheria na taratibu za filamu kabla
ya kuanza kutengeneza na kuzitoa filamu zao ambapo sheria inawataka
kuwasilisha mswada (script) Bodi ili na kupewa idhini yakuendelea na
kazi hiyo.
“Wasanii mnatakiwa kuzingatia sheria na kuwasilisha script ili
zikaguliwe na kupata ruhusa kwa mujibu na taratibu za sheria kabla ya
kuanza kutengeneza filamu kwa sababu sheria Na 4 ya mwaka 1976 ya Filamu
na Michezo ya kuigiza pamoja na kanuni zake zinaelekeza wasanii kutotoa
au kutengeneza filamu kabla ya kupeleka mswada (script ) Bodi ya Filamu
ili ipitiwe.
Aidha Katibu huyo alifafanua kuwa wasanii wanapotengeneza filamu
kupitia script ambazo hazijakaguliwa kuna uwezekano mkubwa wakuwepo
sehemu ambazo zinakiuka maadili ya mtanzania,ikiwepo uvaaji wa mavazi
mafupi yaliyopitiliza kwa waigizaji wanawake,lugha mbaya na baadhi ya
vitendo vingine visivyofaa kuoneshwa kwa umma.
Aliwataka wasanii nchini kutengeneza filamu zinazozingatia maadili ya
Kitanzania ikiwemo kutocheza picha zenye mavazi yanayoopitiliza kwa
ufupi,kubana au zinazoonesha maumbile ya muigizaji mara kwa mara.
Kikao hiki pia kiliwashauri Bodi ya Filamu kukutana na wasanii wa
kike ili kujadili masuala ya mavazi yasiyo nastaha, Bodi imeridhia ombi
hilo.