Umoja wa Mataifa wapitisha Azimio la Kihistoria kuhusu Haki za Watu wenye Albinism
Tarehe 13
Juni, 2013 Baraza la Umoja wa Mataifa la Haki za Binadamu (UNHRC) kwa
pamoja lilipitisha azimio lililowasilishwa na Kikundi cha Umoja wa
Mataifa cha Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza katika ngazi ya
kimataifa kutambua na kushughulikia mashambulizi na ubaguzi dhidi ya
watu wenye albinism katika nchi nyingi.
Azimio
hili la kihistoria limefanikiwa baada ya ushirikiano mkubwa baina ya
Balozi wa Somalia katika Umoja wa Mataifa Mheshimiwa Yusuf Mohamed
Ismail, nchi wanachama zikiongozwa na Kikundi cha Mataifa ya Afrika,
Ofisi ya Kamishna wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu (UNOCHRC) na
Shirika la Under The Same Sun (UTSS).
· Tembelea wavuti zifuatazo kutazama video zinazohusiana na azimio hili la kihistoria: http://www.youtube.com/watch? v=EJIFdT8bKM0&feature=youtu.be
· (UTSS Founder/CEO Peter Ash addresses the UN HRC Assembly on albinism)
· (The Ambassador of Gabon (leader of The African Group of Nations) presents the
resolution to the Council and it is adopted )