Tiketi
za sherehe za kuadhimisha miaka 13 ya muziki wa Lady Jaydee zimeshaanza
kuuzwa mtaani na huo hapo juu na chini ndio mfano wa jinsi zilivyo
ambapo ya juu ni ile ya VIP itakayokuwezesha kupata chakula, nakala ya
CD pamoja na huduma maalum ya kinywaji cha kuanzia
Hii
hapa chini ni ya kawaida itakayokuwezesha kushiriki onesho, na
kushuhudia burudani lukuki zitakazoongizwa na Profesa Jay, TID, Matonya,
Grace Matata pamoja na Lady Jaydee mwenyewe na Machozi Band itaonekana
jukwaani live siku hiyo.
Tiketi
zinapatikaka Shear Illusions-Mlimani City, BM BarberShops-Kinondoni,
City Sports Lounge-City Centre, American Nails-Kinondoni, Nyumbani
Lounge-Tranic Plaza, na katika Bar za Samaki samaki
