Hii ni alama ya barabarani iliyopo eneo la Lwamadovela kata ya Tandala wilaya ya Makete barabara kuu ya Makete-Njombe, ambayo imefutika kwa muda mrefu, kwa hivi sasa ipo kama pambo na haina msaada wowote kwa watumiaji wa barabara hasa madereva! Sijafahamu mara moja nini kimesababisha alama hii kufutika, na tangu ifutike imechukua muda gani, na ilikuwa ikielekeza nini! Ili kuepusha ajali zisizo za lazima tafadhali mamlaka husika zichukue hatua mara moja, maana barabara hutumiwa na madereva wote wakiwemo wageni ambao huenda ni mara yao ya kwanza kutumia barabara hii
DEREVA WA MAKETE, ALAMA HII YA BARABARANI INA MSAADA WOWOTE KWAKO?
By
Unknown
at
Monday, May 06, 2013