Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella
Manyanya pamoja na viongozi wengine wa chama na Serikali pamoja na wadau
mbali mbalimbali na wafanyakazi wakiimba wimbo wa wafanyakazi maarufu
kama "Solidarity Forever" Katika viwanja vya sabasaba mjini Namanyere
Wilayani Nkasi zilipofanyika sherehe hizo kimkoa jana. Kauli mbiu ya
sherehe hizo za Mei Mosi mwaka huu ni "KATIBA MPYA IZINGATIE USAWA NA
HAKI KWA TABAKA LWA WAFANYAKAZI"
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta
wakiangalia maonesho mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na wafanyakazi wa
sekta mbalimbali katika kufanikisha sherehe za Mei Mosi Wilayani Nkasi
zilizofanyika huko kimkoa jana.
Maandamano ya wafanyakazi na mabango
yenye jumbe mbalimbali ilikuwa sehemu ya maadhimisho hayo. Kauli Mbiu ya
sherehe hizo kitaifa ilikuwa "KATIBA MPYA IZINGATIE USAWA NA HAKI KWA
TABAKA LWA WAFANYAKAZI"
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu
Methew Sedoyyeka na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson
Mashala wakiangalia maonesho mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na
wafanyakazi wa sekta mbalimbali katika kufanikisha sherehe za Mei Mosi
Wilayani Nkasi zilizofanyika huko kimkoa jana.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhandisi Stella
Manyanya akitetea jambo na Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Iddi Hassan Kimanta
wakati wa maadhimisho ya siku ya wafanyakazi iliyofanyika kimkoa
Wilayani humo jana.
Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Injinia Stella
Manyanya akimkabidhi cheti na zawadi mmoja ya wafanyakazi bora wa mwaka
2012/2013 katika Ofisi ya Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa Ndugu Elvira
Malema ambaye Sekretari wa Mkuu huyo wa Mkoa jana katika uwanja wa
sabasaba Mjini Namanyere Wilayani Nkasi. Anayeshuhudia kushoto ni Mkuu
wa Wilaya hiyo Iddi Hassan Kimanta.
Michezo mbali mbali ya mpira wa miguu na
netiboli pia ilifanyika ikiwa ni kuhamasisha michezo kwa wafanyakazi
kwa ajili ya kuboresha afya zao kazini na kazi zao kwa ujumla. Mkuu wa
Wilaya ya Sumbawanga kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Rukwa akitoa salam za
Mei Mosi kwa wachezaji wa timu za Veteran Sumbawanga na Namanyere Nkasi
kabla ya kuanza kwa mpambano, timu hizo zilitoa sare 1-1. Kulia ni Mkuu
wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Iddi Hassan Kimanta.Picha na Hamza Temba - Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa