MAKAMU WA RAIS DK. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA 14 WA BARAZA LA USIMAMIZI WA MAWASILIANO AFRIKA, JIJINI DAR LEO


 https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEidkEMhA5g7Yd5eidkvBmEhv9U9BkMUMjrSJnJ37xXc5_0S39LnCKkfij7tqFD-nIwJLGQSOlpfOYmZ41b1ZPKfSgnhpvmCsY8QdB3wdZXPTm7l9q3xZC1ZLk0YTUfGzD4eSvJWlpBFESU/s640/01.jpg

 Makamu wa Rais Dokta Mohamed Gharib Bilal amesema ushirikiano wa kiteknolojia kwa Mataifa ya Kiafrika utasaidia kutamaliza tatizo la uhalifu wa kimtandao.

Dokta Bilal amesema uhalifu huo unasababishwa na ukuaji wa teknolojia na kwamba tatizo hilo litatatuliwa kwa kubadilishana uzoefu na mbinu za kiteknolojia.

Dokta Bilal anatoa suluhisho hilo wakati akifungua mkutano wa 14 wa Umoja wa Mawasiliano wa Nchi za Afrika ATU…

Dokta Bilal ameongeza kuwa bado jitihada zinahitajika kwa kuielekeza vijijini hali itakayosaidia ukuaji wa uchumi wa haraka kwenye Nchi za Afrika kutokana na maeneo hayo kuwa na idadi kubwa ya wananchi.

Profesa Makame Mbalawa ni Waziri wa Mawasiliano Sayansi na Teknolojia anasema serikali inandaa sheria na kanuni za kukabiliana na uhalifu wa njia za kimtandao…

Abdoulkarim Soumaila ni Mwakilishi wa Umoja wa Mawasiliano wa Nchi za Afrika ATU…

Mataifa 14 kutoka Afrika zimeshiriki mkutano huo kwa lengo la kujadili upanuzi wa huduma za kimaendeleo kupitia Sayansi na Teknolojia na namna ya kudhibiti uhalifu unaosababishwa na ukuaji wa teknolojia hiyo kwenye nchi za Afrika.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo