Wananchi wa kata ya Iwawa wilayani Makete ambao wanazitumia
barabara za mitaa zilizokuwa zimelundikwa vifusi kwa muda mrefu, wameipongeza
halmashauri yao kwa kusikia kilio chao na kuanza kusambaza vifusi hivyo hali
iliyopelekea barabara hizo kupitika kirahisi
Hatua hiyo imeokelewa kwa furaha na wakazi hao huku wengine
wakiitaka halmashauri hiyo wakati mwingine kuweka vifusi kwa kulingana na hali
ya hewa ili kuondoa usumbufu wa vifusi hivyo kukaa muda mrefu
Mtandao huu umeshuhudia zoezi la usambazaji vifusi kwenye
barabara hizo likiwa limekamilika na magari yakipita kwani awali barabara hizo
zilifungwa kutokana na matengenezo
Jumatatu ya wiki hii mhandisi wa ujenzi wilaya ya Makete
Eng. Samweli Ndoveni alinukuliwa akisema usambazaji huo wa vifusi utaanza
Jumanne ya wiki hii, ambapo mtandao huu umeshuhudia zoezi hilo likitekelezeka
kama alivyosema




