TAZAMA KATUNI YA KENYA INAYODHALILISHA BUNGE LA TANZANIA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEi8vJnRQvZ2hOMnFR9tmTVIeXvMavBaSjBFtDwocEzYiNcj4pqJ9ry_z6uSJhx0nTUfg2J8-h3Nje1Av51sbQ-XVteSHchuTyIiY-s-lnIlZFyLCzYYL2Kr5KRHexqUWrgPTQaPQXzsagw/s1600/sitta.JPGWaziri wa Afrika Mashariki Mh Samweli Sitta akiwa Bungeni leo amelaani vikali gazeti moja kutoka nchi ya jirani kwa kuruhusu picha hapo juu ambayo imelidhalilisha bunge la tanzania.

Mh Sitta ametoa kauli hiyo leo asubuhi wakati akisoma hotuba ya bajeti ya wizara ya afrika mashariki kwa mwaka 2013/2014.

Sitta amesema pamoja na bunge kuwa na mjadala mkali lakini siyo sahihi Kenya kulidhalilisha bunge la tanzania kwa namna hii na kusema huenda picha hii ikachochea vurugu na majirani zake.

Picha hiyo ilichapishwa katika gazeti moja kutoka kwa majirani zetu siku za hivi karibuni.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo