Mahakama
ya hakimu mkazi manispaa ya Iringa imemuachia huru diwani wa kata ya
mivinjeni FRANK NYALUSI na wenzake watatu JOSEPH MGIMWA,WILLIUM MGUNDA NA
TIMOTHEO MSENJA waliokuwa wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa makosa
matatu.
Akiwasomea
mashtaka yao katika mahakama ya hakimu mkazi mshtakiwa wa pili na
watatu FRANK NYALUSI na JOSEPH MGIMWA wanashtakiwa kwa kosa la
kuwashawishi watu kufanya fujo na kuandamana bila kibali hivyo
kusababisha uvunjwaji wa amani katika barabara ya mashine tatu tarehe 19
mwezi huu.
Wakati
huo huo mahakama imewashtaki watuhumiwa wote (4) kwa kosa la pili la
kuandamana na kufanya mkutano bila kibali cha kamanda mkuu wa jehi la
polisi hivyo kusababisha vurugu katika eneo la mashine tatu,na kosa la
tatu mahakama ime washtaki watuhumiwa na 2 na namba tatu kwa kosa la
kushawishi watu kufanya fujo na kufanya uhalibifu wa mali likiwemo gari
la kikosi cha zima moto mkoani hapa.
Washitakiwa
wote wameachiwa huru kwa dhamana ya shilingi milioni 1 huku mahakama
ikiwataka washitakiwa wa nne kuto jihusisha na sehemu yoyote yenye
dalili ya uvunjwaji wa amani.
