TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA SINGIDA



Taarifa Kwa Vyombo Vya Habari

Taasisi ya Hassan Maajar Trust na Shirika La Nyumba La Taifa Watoa Msaada Wa Madawati Singida

Tarehe 27 Aprili 2013 - Singida. Zaidi ya wanafunzi 750 katika shule saba za wilaya ya Singida zitapokea msaada wa madawati yaliyotolewa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust na Shirika La Nyumba La Taifa  

Jumla ya madawati 264 yanatolewa na wabia hao kupunguza tatizo sugu la upungu wa madawati katika shule hizo. Hafla ya kukakabidhi madawati hao, imefanyika katika Shule ya Msingi ya Munisa, iliyoko Halmashauri ya Singida.  Bwana Shariff Maajar, kwa niaba ya Taasisi ya Hassan Maajar Trust akishirikiana na Bwana Nehemiah Mchechu kwa niaba ya Shirika La Nyumba La Taifa, walikabidhi madawati hayo kwa Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Parseko V Kone. 

“Napenda kutoa shukurani za dhati kwa Wakfu wa Hassan Maajar na Shirika La Nyumba La Taifa kwa msaada hu mkubwa utakaochangia kuboresha elimu Singida’, alisema Dr. Kone.  Wanafunzi mkoani Singida, hususan, walioko vijijini wanakabiliwa na changamoto kubwa la kwanza likuwa mazingira ya kusomea, hivyo tunafarijika kuona wabia wanotusaidia kuboresha mazingira ya elimu kwa watoto wetu. Hii inakuza viwango na kuhimiza matokeo bora”, aliongeza. 

Chini wa mradi wa Hassan Maajar Trust wa “Dawati Kwa Kila Mtoto”, (A Desk For Every Child) mkoa wa Singida wa pili kati ya mitano itakayonufaika kwa msaada inyaotelewa na Hassan Maajar Trust kwa kutumia fedha zilizopatikana na michango iliyotolewa kufwatia kampeni iliyoanzishwa Desemba 2011. Garama za madawati haya ni Tsh 22,500,000, kati ya hizo Shirika La Nyumba La Taifa limetoa jumla ya Tsh 10,000,000. 

“Tunataka kuhakikisha kuwa kampeni ya Dawati Kwa Kila Mtoto inawafikia watoto wengi iwezekenavyo na kujenga maisha bora kwa watoto hao”, alisema Zena Tenga, Mkurugenzi Mtendaji. “Tunashukuru Shirika La Nyumba La Taifa kwa kuunga mkono juhudi zetu. Tutaendelea kuhamasisha ushirikiano na wote wenye nia ya kuona lengo la Hassan Maajar Trust la kuhakikisha watoto wetu wakiondoka sakafuni na kukaa kwenye madawati lina timia”,aliongeza.

 “Tunafurahi kuona kwamba mchango wa shirika letu sasa uko katika hali ya madawati ambapo watoto watakaa na watafurahia masomo ‘, alisema Bw. Mchechu, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika La Nyumba La Taifa.   , “ Shirika la Nyumba La Taifa lilishirikiana vema na Taasisi ya Hassan Maajar Trust kuchangia fursa hii adimu kwa wanafunzi na maendeleo ya elimu kwa ujumla”, aliongeza.

Kuhusu Hassan Maajar Trust
Taasisi ya Hassan Maajar Trust imeandikishwa kama kampuni au NGO isiyo na hisa na yenye kudhaminiwa na kufanya kazi za hisani bila faida. Lengo kuu la Taasisi ya Hassan Maajar Trust ni kuboresha mazingira ya elimu katika shule za Tanzania.


Kuhusu Shirika La Nyumba La Taifa
Malengo ya Shirika la Nyumba la Taifa ni kuwa kampuni bora katika kuendeleza na kusimamia ujenzi wa nyumba na majengo mengine yenye ubora kwa matumizi ya umma. Ikifanya kazi katika misingi sahihi na imara ya kibiashara. 
Kwa maelezo zaidi tembelea : www.nhctz.com

Imetolewa na: PR-Aggrey & Clifford • Mobile +255 772 131 367


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo