WAZIRI NCHIMBI ASEMA WAPINZANI NI ZAIDI YA WACHAWI

Waziri Emmanuel Nchimbi

Katika hali isiyokuwa ya kawaida baada ya msemaji wa kambi rasmi ya upinzania Bungeni kuhusu wizara ya maliasili na utalii kumaliza kusoma hotuba ya kambi hiyo na kuwatuhumu baadhi ya viongozi na makada wa CCM kuhusika moja kwa moja kuihujumu wizara hiyo na kujinufaisha wao wenyewe

waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Emmanuel Nchimbi amesimama na kuwatolea maneno makali akidai kambi rasmi ya upinzani ni genge la waongo na wazushi wenye madhara makubwa katika jamii kuliko wachawi wenye maono mafupi.
"MHESHIMIWA SPIKA,kilichojidhihirisha siku za karibuni ni kwamba Kambi ya upinzani imeamua kwa makusudi kuanza kutazama maono yao kwa mtazamo mfupi usiojali maslahi ya taifa letu....wameamua kufanya siasa za kupakana matope,siasa za kuchafua watu,siasa za kutunga uongo,siasa za uzushi,siasa za kutoana kucha(kumbe yeye kama waziri wa mambo ya ndani anajua watoaji kucha) na kila aina ya siasa ambazo zinaichafua nchi yetu(makofi mazito kutoka upande wake)....mheshimiwa spika,bunge lako ni lazima likatae utaratibu huo,haya ni maono mafupi na maono ya watu wasiotazama mbele....hivi leo tukiwakabidhi serikali na kama mchezo wao ndio huu watafanya ninii?...

akaendelea zaidi mh.Nchimbi.....Mheshimiwa spika mimi ni mkristo na biblia inasema ni afadhali mchawi kuliko muongo(sina uhakika kama kuna kipengele hicho kwenye biblia)...

mheshimiwa spika,kwenye bunge lako tumekaa na genge la watu waongo ambao wanaweza wakasababisha maafa zaidi ya uchawi katika nchi yetu...(kuhusu utaratibu...kuhusu utaratibu mheshimiwa spika...ilisikika sauti kutoka upinzani...spika akajibu..muache kwanza amalize"akaendelea mbele ila hivyo ndivyo hali ilivyokua bungeni hii leo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo