MKALI wa filamu na muziki Bongo, Snura Mushi amesema anaogopa kuingia
kwenye uhusiano wa kimapenzi na wasanii wa filamu kwani wengi wao hawana
mapenzi ya kweli.
Akipiga domo na paparazi wetu, Snura alisema tangu aanze kucheza filamu alijiapiza kuwa kamwe hatajiingiza kwenye mapenzi na waigizaji zaidi ya kushirikiana nao katika kazi ya kuzalisha filamu.
Akipiga domo na paparazi wetu, Snura alisema tangu aanze kucheza filamu alijiapiza kuwa kamwe hatajiingiza kwenye mapenzi na waigizaji zaidi ya kushirikiana nao katika kazi ya kuzalisha filamu.
“Mimi siwapendi wanaume wasanii wa filamu, sijawahi kuwa nao labda awe msanii wa Bongo Fleva,” alisema Snura.