Mmoja wa majeruhi katika jengo la
ghorofa 16 lililodondoka katika Mtaa wa Indira Ghandhi juzi jijini Dar
es Salaam, ameelezea jinsi alivyonusurika kifo katika ajali hiyo akiwa
ghorofa ya 15.
Selemani Said (26) ambaye ni miongoni mwa majeruhi wanne waliolazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) anasema wakati akiwa gorofa ya 15 alishuhudia jengo lilivyokuwa likianza kushuka.
Selemani Said (26) ambaye ni miongoni mwa majeruhi wanne waliolazwa katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI) anasema wakati akiwa gorofa ya 15 alishuhudia jengo lilivyokuwa likianza kushuka.
Majeruhi huyo ambaye ni fundi ujenzi, alisema wakati ajali hiyo ikitokea asubuhi, alishuka na jengo hilo hadi chini na baada ya hapo, alipoteza fahamu na kushtukia akiwa hospitali.
“Siku ile ilikuwa ni siku ya kumwaga zege. Tulikuwa wengi wakiwemo vibarua ambao jengo linapofikia hatua ya kumwaga zege, huwa linahitaji vibarua wengi, nikiwa najiandaa kuanza ujenzi, mara nilihisi kama jengo linaanguka, nilipoangalia nje niliona ninashuka nalo,” alisema Said.