Mechi namba 163 ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyochezwa juzi (Aprili 28
mwaka huu) kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na kumalizika kwa Simba
kuibuka ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Polisi Morogoro imeingiza sh.
18,014,000.
Watazamaji 3,145 walikata tiketi kushuhudia mechi hiyo ambayo viingilio vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 3,564,252.45 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 2,747,898.31.
Mgawo mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 1,812,331.75, tiketi sh. 3,183,890, gharama za mechi sh. 1,087,399.05, Kamati ya Ligi sh. 1,087,399.05, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 543,699.53 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) sh. 422,877.41.
Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)