Muigizaji wa filamu Halima Yahaya ‘Davina’ amejifungua mtoto wa kiume
katika Hospitali ya Aga Khan hivi karibuni.
Msanii huyo mahiri katika
tasmia ya filamu nchini Tanzania alikuwa amejawa na furaha wakati
alipotembelewa na wa wasanii wenzake kwa ajili ya kumjulia hali na kumpa
hongera.
Namshukuru “mwenyezi Mungu kwa kujifungua salama na nimepata Baby boy
nimefurahi sana unajua siku mambo ya uzazi yanavyokuwa lakini pia
asante kwa nyinyi rafiki zangu kuja kunitembelea na kujua hali yangu na
mimi nipo salama kabisa na mtoto yupo sawa,” alisema Davina. Davina
alitembelewa na wasanii wenzake katika Hospitali ya Aga khan kumpongeza.
Baadhi ya wasanii hao walioenda kumuona ni Jenifer Kyaka ‘Odama’,
Salama Salmin ‘Sandra’, na kiongozi wa kundi la Bongo movie Herith
Chumila, wanaonekana pichani chini wakiwa wenye furaha kwa rafiki yao
kujifungua salama na kuwaletea mtoto wa kiume.
Source: Pro-24
Source: Pro-24