KAJALA AJICHORA TATOO YA WEMA


.
Siku kadhaa baada ya mwigizaji Wema Sepetu kulipa milioni 13 na kumalizana na faini iliyokua inamkabili mwigizaji Kajala aliyotakiwa kulipa Mahakamani baada ya kupatikana na hatia kwenye kesi yake, mwigizaji Kajala alieguswa na wema wa Wema, ameamua kochora mgongoni tattoo ya jina la Wema.


Wema Sepetu amesema kwamba Kajala alikwenda nyumbani kwake na kuchora hii tattoo bila kumwambia, Wema alipouliza kuna nini mbona kama kuna kitu kinaendelea, Kajala alimwambia mtu wa Tatoo asimwambie mpaka walipomaliza kuchora ndio wakamwonesha huku Kajala akimwambia Wema ni shujaa wake kwa alichofanya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo