WADAU WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI WALAANI VITENDO VYA KUTEKWA, KUTESWA NA KUUAWA KWA WANAHABARI NCHINI

Wadau wa vyombo vya habari nchini wamelaani hatua ya kutekwa, kuteswa na kuuawa kwa wanahabari, huku wakidai kuwa mateso ya Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, kumetokana na msimamo imara wa kalamu yake. 

Wadau hao wakiongozwa na Chama Cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari nchini (MOAT), Baraza la Habari Tanzania(MCT) na Jukwaa la Wahariri, Wamesema shambulio lililofanywa dhidi ya Kibanda halikutokana na kitu kingine chochote, zaidi ya kazi yake ya uandishi  wa habari.  

Kutokana na hali hiyo, wadau hao wamelichukua suala hilo kuwa ni shambulizi dhidi ya uhuru wa vyombo vya habari nchini na kuwajengea hofu wahariri, waandishi na wanaharakati wote ili wasitekeleze wajibu wao kwa umma.

Wakizungumza kwa kupokezana, wamesema tukio hilo ni mfululizo wa mashambulizi ya ambayo yamejitokeza kwa vipindi tofauti ikianza kwa waandishi wa habari wa gazeti la Mwanahalisi, Saed Kubenea na Ndimara Tegambwage, kutekwa kwa Dk. Steven Ulimboka, kuuawa kwa mwandishi wa kituo cha Channel Ten, Daudi Mwangosi, na sasa mashambulizi dhidi ya Kibanda.Wameitaka Serikali kuunda tume huru ya wapelelezi ili kuchunguza undani wa masuala hayo, kwa kuwa kasi ya uchunguzi wa vyombo vya usalama hapa nchini hairidhishi na pia baadhi ya watendaji  ndani ya vyombo hivyo wanahusishwa na kadhia hizi


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo