SERIKALI MKOANI MBEYA YAZUNGUMZIA TUHUMA ZINAZOWAKABILI WALIMU WALIOKAMATWA NA TAKUKURU


logo
Hatimaye serikali mkoani Mbeya, imevunja ukimya na kuzungumzia hatua zinazokusudiwa kuchukuliwa dhidi ya uongozi wa shule ya sekondari Forest ya Jijini Mbeya, wanaodaiwa kutumia moja ya chumba katika ofisi za shule hiyo kutoa adhabu kwa wanafunzi wanaoshindwa kutoa hongo ya shilingi 500 hadi 1000 kwa makosa mbalimbali ikiwemo kuchelewa. 

Siku ya Jumatatu Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini (Takukuru) mkoa wa Mbeya iliwakamata walimu wawili, Faustini Robert na Josephat Mwasote, kwa tuhuma za kushawishi na kuomba rushwa ya kati ya shilingi 500 hadi 1000 kwa wanafunzi ambao huchelewa kufika shuleni.

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake, Afisa elimu Mkoani Humo, Juma Kaponda, amesema baada ya serikali kupokea taarifa hizo za kusikitisha imeanza kufanya uchunguzi wa kubaini ukweli wake ili iweze kuchukua hatua kali za kukomesha tabia hizo.

Amesema watahakikisha wale wote waliohusika na tuhuma hizo wakiwemo viongozi wa shule wanachukuliwa hatua kali za kinidhamu kwa kuwa taarifa zinaonesha tatizo hilo limefanyika kwa muda mrefu shuleni hapo.

Kufuatia tuhuma hizoKaponda amekutana na maofisa elimu wa Jiji la Mbeya ili kupata taarifa za kina juu ya tukio hilo na kama walikuwa na taarifa za aina hiyo ambazo ni kinyume na utumishi wa umma.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo