Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akiwaonyesha wadau
mbalimbali wa haki za binadamu na utawala bura kijitabu cha mambo 101
unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza mara
baada ya kukizindua kitabu hicho leo katika ukumbi wa mikutano wa
ofisi za Tume ya Haki ya Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento
akifuatiwa na Katibu Mtendaji wa Tume Mary Massay.PICHA NA ANNA NKINDA
Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akizindua kijitabu cha
mambo 101 unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza
leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya Haki ya Binadamu na
Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimeandaliwa na Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ubalozi wa Uingereza Nchini na Taasisi
ya Jumuia ya Madola inayoshughulikia haki za binadamu. Kutoka kushoto
ni Mwenyekiti wa Tume hiyo Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento
akifuatiwa na Katibu Mtendaji wa Tume Mary Massay.
Wadau
mbalimbali wa haki za binadamu na utawala bora wakiwa katika picha ya
pamoja mara baada ya kumalizika kwa uzinduzi wa kitabu cha mambo 101
unayohitaji kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza
uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya Haki ya
Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kitabu hicho kimeandaliwa
na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ubalozi wa Uingereza
Nchini na Taasisiya ya Jumuia ya Madola inayoshughulikia haki za
binadamu.
Naibu
Balozi wa Uingereza nchini Julian Chandler akielezea jinsi nchi yake
ilivyoona umuhimu wa kuandaa kitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu
kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza wakati wa uzinduzi wa kitabu
hicho uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu
Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki akifuatiwa Mwenyekiti wa
Tume hiyo Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri Manento.
Katibu
Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Mary Massay
akielezea kuhusu uzinduzi wa kitabu cha maswali 101 unayohitaji
kuyafahamu kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza wakati wa uzinduzi wa
kitabu hicho uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za
Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kitabu
hicho kimeandaliwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Ubalozi
wa Uingereza Nchini na Taasisiya ya Jumuia ya Madola inayoshughulikia
haki za binadamu.
Mwenyekiti
wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora Jaji Kiongozi Mstaafu Amiri
Manento akielezea jinsi kitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu
kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza kitakavyowasaidia wananchi kujua
haki zao za msingi wakati wa uzinduzi wa kitabu hicho uliofanyika leo
katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume hiyo jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Naibu Waziri wa Katiba na Sheria Angellah Kairuki na kushoto ni
Katibu Mtendaji wa Tume hiyo Mary Massay.
Mkurugenzi
wa Taasisi ya Jumuia ya Madola inayoshughulikia haki za binadamu Sarah
Mount akielezea umuhimu wa kitabu cha mambo 101 unayohitaji kuyafahamu
kuhusu Polisi lakini unaogopa kuyauliza wakati wa uzinduzi wa kitabu
hicho uliofanyika leo katika ukumbi wa mikutano wa ofisi za Tume ya
Haki za Binadamu na Utawala Bora jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Kamishna wa Tume hiyo Bernadeta Gambishi.