CHAMA CHA WASIOONA IDARA YA WANAWAKE CHATAKA WANAWAKE WASIOONA WASHIRIKISHWE MCHAKATO WA KATIBA

    DSC05398    
Na Immaculata Makilika na Lorietha Laurence Maelezo

CHAMA  cha wasioona Tanzania  idara ya wanawake  kimetoa wito kwa wanajamii  na wadau mbalimbali kushirikisha  wasioona katika mchakato wa uundwaji wa Katiba mpya nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mweyekiti wa Chama cha Wasioona Idara ya Wanawake   amesema kuwa  wanawake wakishirikishwa katika uundwaji wa katiba mpya watakuwa na sauti moja katika kudai maslahi yao.

Ameeleza kuwa lengo kuu ni kuwawezesha wanawake kuwa na sauti moja katika  kudai maslahi yao hasa masuala muhimu yanayowahusu wasioona kama jamii yenye mahitaji sawa na wengine.

“Wanawake wasioona wakipewa nafasi katika katiba mpya wataweza kutambuliwa na kuthaminiwa katika masuala yote ya kijamii kama vile, siasa, elimu,uchumi na Utamaduni.”Alisema Bi. Kulangwa.

Wakati huohuo Katibu wa chama hicho Bi. Doroth Kaihuzi amehamasisha jamii ichangie katika harakati  za maendeleo  kwa wasioona  katika nyanja mbalimbali ikiwemo uhamasishaji juu ya mchakato wa uundwaji wa katiba mpya.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo