LOWASSA AMPONGEZA PAPA MPYA

 
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Monduli, Edward Lowassa ametoa salamu za pongezi kwa Papa Mpya wa Kanisa Katoliki Duniani, Papa Francis I kwa kuchaguliwa kuliongoza Kanisa hilo Duniani.

Lowassa ametuma salamu hizo kwa Papa kupitia ukurasa wake wa Facebook na pia ametoa pongezi kwa Wakatoliki wote Duniani kwa kumpata Kiongozi huyo ambaye kiasili na jina lake ni Mt. Francis ni mtu wa kawaida.

Huu ndio ujumbe Kamili aliyouandika Ndugu, Edward Lowassa katika Ukurasa wake huo:-

“Hongera Cardinal Jorge Mario Bergoglio kwa kuchaguliwa kuwa Pope Francis I,

Na pia hongera wakatoliki wote duniani zaidi ya bilion 1 kwa kumpata Kiongozi ambaye kiasili na jina alilolichagua la Mt Francis ni mtu aliyeishi maisha ya kawaida na ya kuwapenda masikini katika maisha yake yote ya uitumishi.

Naamini sasa dunia mpya ya watu masikini kupata tumaini la maisha imezaliwa, na kwa pamoja tuungane kumpongeza na kumtakia mafanikio mema kiongozi wetu mkuu wa Kanisa katoliki duniani.

Na pia Roho mtakatifu amwongoze katika kuzikabili changamoto za kanisa duniani kote.” Alimalizia Lowassa katika Ujumbe huo.

ASANTENI SANA.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo