
Na Sufiani Mafoto
WACHEZAJI
watatu wa klabu ya DC Motema pembe-DCMP ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Congo-DRC wamefariki dunia kwa ajali ya gari iliyotokea jijini Kinshasa
jana.
Wachezaji
hao ambao ni golikipa Guelor Dibulana, washambuliaji Hugues Muyenge na
Mozart Mwanza walikuwa wakirejea kutoka katika Ibada maalum ya Ijumaa
Kuu kuelekea Pasaka, iliyofanyika katika kanisa la Saint- Dominique
lililopo Kinshasa.
Imeelezwa kuwa ajali hiyo imetokea baada ya gari lao walilokuwamo kugongwa na Lori.
Kwa
mujibu wa taarifa za hospitali mchezaji mwenzao Mbindi ambaye alikuwa
akiendesha gari hilo alisalimika pamoja na abiria mwingine huku wao
wakiwa wamepata majeraha makubwa.
DCMP ilitarajiwa kucheza na timu ya AS Vita Club leo jumalipi.