Mkazi wa kijiji cha Matenga wilayani Makete ambaye jina lake halikupatikana mara moja akiweka mafuta kwenye pikipiki huku akiwa amepakiza abiria wawili(mishikaki) bila kujali usalama wake na abiria aliowabeba
baada ya kuweka kiwese hapa anachukua hela yake, lita moja ya mafuta kijijini hapo huuzwa sh.2800/-
Wakazi wa kijiji cha Ikuwo wilayani Makete wakitafuta mtandao wa simu katika eneo maarufu lenye mtandao wa simu katika Zahanati ya kijiji hicho. Kijiji cha Ikuwo ni kijiji chenye ukosefu wa mtandao wa simu zote kwa maana rahisi hakuna mtandao kabisa, labda uje eneo hilo
Kijiji cha Ikuwo
Viongozi wa vijiji vya tarafa ya Ikuwo wilayani Makete wakifurahia kugawiwa bure maboksi ya kondomu kutoka shirika la SUMASESU lililotembelea kijijini hapo kama namna mojawapo ya mapambano dhidi ya VVU/UKIMWI