Matokeo yaKidato cha Nne ya namna hii (zaidi ya nusu ya wahitimu
kupata sifuri) na takribani asilimia 90 kufeli kwa kupata daraja la nne
na daraja la sifuri ni mwaka tatu sasa mfululizo. Matokeo yakitoka
tunasema weeee mpaka povu linatoka. Baada ya wiki tumeshasahau na hakuna
hatua yeyote. Lazima Uwajibikaji utokee.
kwanza
Waziri lazima awajibike na Naibu wake na Katibu Mkuu na Kamishna. Najua
kuwa haina uhusiano wa moja kwa moja maana matatizo ya elimu ni makubwa
sana nchini. Lakini ni lazima kitu fulani kitokee ili kufanya
mabadiliko. Uwajibikaji ni njia mojawapo inayoleta nidhamu na ‘urgency’
katika utendaji kazi.
Tumwambie Rais aichukue Wizara ya Elimu,
yaani Waziri wa Elimu awe yeye (kuwe na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais
Elimu). Tumwambie matokeo yakibaki hivi mwakani na yeye atatoka.
Najua
wa mwakani ndio wapo kidato cha nne sasa na wana msingi mbaya tayari
lakini sio jukumu letu kujipa majibu bali ni jukumu letu kuiambia
Serikali hapana. Tuwape Masharti. Vinginevyo haya yatakwisha na mwakani
itakuja nk. ZAIDI BOFYA HAPA: http://lindiyetu.blogspot.com/2013/02/zito-kabwe-afunguka-live-kuhusu-matokeo.html