Fundi
wa Shirika la Umeme Tanesco mkoani Iringa, Selemani Mbuma akiwa
amenaswa na umeme baada ya wenzake kuwasha umeme kimakosa wakati
akiendelea na matengenezo katika eneo la Mlandege mkoani humo.
Matatizo
haya hujitokeza mara kwa mara Je swali la kujiuliza huwa hawawasiliani
pindi wanapotaka kurudisha umeme huo? au hakuna fundi in charge ambaye
ndio kiongozi wa msafara wa ufundi ambaye ndie atakaye husika na
miongozo yote ya kuhakikisha kuwa hakuna mtu anaye endelea na
matengenezo ndio umeme uwashwe? jibu naweza jipa mwenyewe kuwa lazima
awepo ila ni Ufanyaji kazi wa mazoea na kuwaamini sana hawa wanaoitwa
saidia kuwapa majukumu yaliyokuwa makubwa kuliko uwezo wao na ndio
makosa kama haya yanatokea, maisha ya mtu yanapotea kwa uzembe wa
kizembe kama huu.
Picha na Geofrey Nyang’oro