mji wa Kyela
Na Ibrahim Yassin,Kyela
SERIKALI wilayani Kyela mkoani Mbeya imeshitushwa na idadi
kubwa ya vifo vitokanavyo na watu kujinyonga wenyewe sambamba na vifo
vitokanavyo na imani za kishirikina
Hayo yamebainishwa kwenye baraza la madiwani
lililofanyika jana katika ukumbi wa halmashauri ya wilaya ambapo mkuu wa wilaya
Kyela ,Magreth Malenga alisema kuwa ameshitushwa na wimbi la watu wengi
kujinyonga na mauaji yatokanayo na imani za kishirikina
Alisema kuwa hivi karibuni katika kijiji cha Ushirika kitongoji cha Ibungumbati Mwanafunzi wa
darasa la sita aliuawa kinyama na baadhi ya viungo vyake kuchukuliwa kwa imani
za kishirikina na kuwa hari hiyo siyo nzuri inaharibu hari ya utulivu tulionao
na kuwa ipo haja ya kuchukua hatua ili vitendo hivyo visiweze kupewa nafasi na
kila mmoja kulaani hari hiyo
Mkuu huyo wa wilaya alisema katika mkoa Mbeya wilaya Kyela
inaongoza kwa vifo vingi vitokanavyo na watu kuamua kujinyonga na ukifuatilia
kwa kina sababu za watu wengi kuamua kujinyonga ni masuala ya mapenzi na kidogo
ugumu wa maisha,hivyo amewataka madiwani na wadau wengine kuwaelimisha wananchi
namna ya kutafuta suluhisho la matatizo yao kwa njia nyingine badala ya
kujinyonga kama wanavyofanya sasa
Pia mkuu huyo wa wilaya alipata fursa ya kulizungumzia kwa
kina suala la matokeo mabaya ya kidato cha nne yaliyotangazwa hivi karibuni na
waziri wa elimu na mafunzo ya ufundi Dkt,Shukuru Kawambwa ambapo sasa ameiagiza
halmashauri ikae na kujitathimini juu ya matokeo hayo na kujipanga sawasawa
hasa katika shule za msingi
Hivyo amemuagiza afisa elimu wa shule za msingi kuwa walimu
wapya watakaolipoti mwaka huu wote wapelekwe katika shule zilizopo vijijini
kwani huko ndiko kwenye mahitaji halisi ya walimu ukilinganisha na shule
zilizopo vijijini
Alisema shule za msingi nyingi mazingira yake ya kujifunzia
si mazuri na kuwa hivi karibuni alifanya
ziara ya kushitukiza katika baadhi ya shule za msingi vijijini na kukuta hari
ni mbaya kwani baadhi ya shule hazina vyoo na matatizo mengi na kuwataka
madiwani kuwashirikisha wananchi wao katika kutatua kero mbalimbali kama hizo
na kuwa hilo linawezekana kama wananchi watashirikishwa na michango yao
ikafanya kazi inayokusudiwa
Baraza hilo la madiwani liliweza kupitisha taarifa ya mapato
na matumizi ikionyesha bajeti timilizi kwa kipindi cha robo ya pili ya mwaka
toka Disemba 2012/13 ambapo halmashauri imeweza kukusanya 2,140,565,687.32 kwa mchanuo mbalimbali
ikiwemo makusanyo ya ndani,Ruzuku ya mishahara na Ruzuku ya serikali kuu