Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, wilaya ya Lindi mjini, Mke wa
Rais Mama Salma Kikwete akikagua mtaro katika mtaa wa Wailes Lindi
mjini, leo. Mtaro huo unadaiwa kusababisha maafa ya mafuriko kuua watoto
watano mwaka jana, kutokana na kumwaga maji mitaani wakati wa mvua
badala ya kufuata mkondo wa mtaro. Mama Salma amewapa pole waliopoteza
watoto wao na kuagiza Halmashauri ya wilaya hiyo kusimamia ili mtaro huo
ujengwe kwa kiwango kinachotakiwa.
Vijana wakila kiapo baada ya kukabishiwa kadi zao za UVCCM na Mjumbe wa
Halmashauri Kuu ya Taifa, Mama Salma Kikwete kwenye mkutano uliofanyika
Kata ya Waile Lindi mjini.
Mzee Ismail Bakari (80) maarufu kwa jina la Kulombandila akimuuliza
swali mama Salma Kikwete kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye
Ofisi ya CCM, wilaya ya Lindi mjini leo.
Kina mama wa Kata ya Mikumbi Lindi wakimpa zawadi ya mkeka Mama Salma
Kikwete kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika leo kwenye kata hiyo.
Wananchi wakiwa kwenye Mkutano wa Kata ya Kikumbi
Hashim Masoud kutoka CUF akikabishi kadi yake kwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete baada ya kaumua kujiunga na CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Mikumbi, leo. Wanachama 25 wakiwemo watano kutoka CUF walijiunga CCM. Picha na CCMBLOG