IRINGA PRESS CLUB YAKABIDHIWA VIFAA VYA KISASA NA UTPC


 Makamu  mwenyekiti  wa umoja  wa vilabu  vya  waandishi  wa habari Tanzania (UTPC) Jane Mihanji akimkabidhi katibu mtendaji  wa IPC Francis Godwin seti ya  TV ya  kisasa kwa ajili ya matumizi ya IPC

Na Francis Godwin
KLABU ya  waandishi  wa habari mkoa  wa Iringa (IPC) imepongeza utendaji kazi  wa bodi nzima ya umoja  wa vilabu  vya waandishi  wa habari Tanzania (UTPC) chini ya Rais wake Keneth Simbaya na mkurugenzi Abubakar Karsani.

Akitoa pongezi  hizo leo katika ofisi  wa Klabu ya  waandishi  wa habari mkoa  wa Dar es Salaam ofisi za Dar City Press Club mara  baada ya  kukabidhiwa vifaa mbali mbali  vya mamilioni ya shilingi kwa ajili ya kuboresha utendaji kazi  wa  wanachama  wake katibu  mtendaji  wa IPC Francis Godwin alisema  kuwa kwa muda wanahabari  walikuwa wakifanya kazi kwa kutegemea vitendea kazi duni  hivyo hatua ya UTPC kuanzisha mpango huo  wa  kuvisaidia vilabu vya waandishi  wa habari nchini ni moja kati ya mambo ya  kujipongeza na kupongeza watendaji  wa UTPC kwa kuwa na mtazamo wenye kuboresha  zaidi vilabu vya wanahabari.

Godwin  alisema  kuwa vifaa hivyo ambavyo ni pamoja na kamera za picha vya mnato na video vitawezesha  wananchi  mkoa  wa Iringa  kupiga hatua  zaidi katika  utendaji  kazi  wao  wa kila  siku .
  
 Ofisa Mipango wa UTPC, Jacob Kambili, alivitaja  vifaa mbavyo IPC imekabidhiwa na UTPC  kuwa ni pamoja na Desktop Computer ,Desktop Monitor , Printer ,Laptop, UPs ,Binding Machine,Lamination Machine , Photcopy Machine, Multimedia Projector , Professionl Still Camera,DVD Palayer, TV Set Video Camera Radio Reeciver Sony, Collapsible Screen  electric Screen  na Recoda na kuwa  vitu  vyote hivyo  vikiwa na thamani ya zaidi ya shilingi milioni 35.

Alisema kuwa lengo la  vifaa hivyo ni kuwawezesha  wanachama wote  wa IPC  kuweza kunufaika na vifaa hivyo katika  utendaji kazi  wao na  kuwa kila mwanachama wa  IPC anayonafasi ya  kuvitumia vifaa hivyo na si mali ya viongozi  wa IPC.

"Nawaombeni  sana viongozi  wa IPC na viongozi  wa vilabu vyote  vya waandishi  wa habari nchini ambao tayari  mmepewa vifaa hivi kuhakikisha haki inatendeka katika kuviazimisha  kwa  wanachama badala ya  kuhodhi viongozi pekee "alisema

Siku  zote  chokochoko katika vilabu  vingi hapa nchini huanza  kujitokeza katika mafanikio na kuwa hata  pale ambapo palikuwa hakuna migogoro baada ya  kuanza kuona mafanikio ndipo  wanachama huanzisha  migongano jambo ambalo asingependa kulisikia katika vilabu  hivyo  vya wanahabari nchini.

Hata  hivyo alisema ili kujenga chama chenye  wanachama wanaozingatia maadili ni vema viongozi kusimamia usawa na haki katika utendaji na kutoruhusu migongano isiyokuwa ya kawaida ndani ya klabu.

Pia  aliwataka  viongozi  wa IPC  kwa sasa baada ya  tukio  la mauwaji ya aliyekuwa mwandishi  wa habari wa IPC Marehemu Daudi Mwangosi kujipanga upya kuendelea kufanya kazi hiyo pamoja na kusimamia vema IPC 

Kwa upande  wake makamu  wa Rais  wa UTPC Jane Mihanji alisema kuwa lengo la UTPC  kutoa  vifaa hivyo ni  kuviwezesha  vilabu  vya wanahabari kwenda kisasa  zaidi na kuwa UTPC imekuwa ikiviwezesha vilabu  hivyo vya  wanahabari nchini katika nyanja mbali  mbali ikiwa ni pamoja na kutoa mafunzo mbali mbali kama njia ya kuboresha  maadili ya uandishi  wa habari nchini.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo