skip to main |
skip to sidebar
WATATU WAKAMATWA KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA MAUAJI YA PADRI MUSHI
MAKACHERO
wa Jeshi la Polisi nchini wamewatia mbaroni vijana watatu wanaotuhumiwa
kuhusika katika mauaji ya Padri Everist Mushi (55) wa Kanisa Katoliki
mjini Zanzibar.
Watuhumiwa hao wamekamatwa mjini Nairobi, Kenya
kutokana na ushirikiano wa Jeshi la Polisi la Tanzania na Polisi wa
Kenya kwa mwamvuli wa Shirikisho la Polisi wa Kimataifa (Interpol).
Habari za kuaminika kutoka Nairobi, Kenya zimesema kuwa watuhumiwa hao
ambao majina yao yamehifadhiwa, walitiwa nguvuni juzi mjini humo
walipowasili wakitokea Mombasa, mashariki mwa nchi hiyo.
Watuhumiwa hao ambao walikuwa wakiingia katika maficho kukwepa mkono wa
dola, wanadaiwa kutumia jahazi kusafiria kutoka Zanzibar hadi Mombasa,
Kenya kabla ya kusafiri kwa magari hadi Nairobi ambako walitiwa nguvuni.
Habari na Jamii Forums.
JIUNGE NA EDMO BLOG SASA
Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube
Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi