Na Walter Mguluchuma-BLOGS ZA MIKOA Mpanda
Majambazi
wameliteka gari la mfanya biashara wa duka la dawa muhimu la
binadamu wa Mjini Mpanda Mkoa wa Katavi Michael Mpela na kufanikiwa
kupora vitu vyenye thamani ya shilingi 480 000.
Kaimu
kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi Joseph Myovela alisema tukio
hilo la uporaji lilitokeaa februari 8 majira ya saa 2 usiku katika
eneo la Kijiji cha Sijonga barabara ya Mpanda kuelekea Karema
mwambao wa ziwa Tanganyika .
Katika
tukio hili majambazi watatu wakiwa na bunduki moja waliliteka
gari namba T 595 AGS aina Escudo mali ya Michael Mpela aliye kuwa
na wenzake wawili.
Kaimu
kamanda wa polisi wa mkoa wa Katavi alisema baada ya kuwateka
walifanikiwa kuwapora pesa taslimu jumla ya shilingi 240 000.
pia
majambazi hao waliwalazimisha kusalisha simu zao za mikononi na
waliweza kupora simu tano za aina mbambali zenye thamani ya
shilingi 240 000.
Myovela alisema majambazi hayo mara baada ya kufanya ujambazi huo yalitokomea kichakani na kutokomea kusiko julikana .
Alieleza
jeshi la polisi linaendelea na msako wa kuwatafuta mambazi walio
husika katika tukio hili kwa kushirikiana na wananchi .
Na
jeshi la polisi mkoa wa Katavi limetowa wito kwa kwa wananchi
kutowa taarifa mapema waonapo watu ambao ni wageni katika
maeneo yao wanapo kuwa na mashaka nao kabla hawaja fanya adhima
yao ya uharifu