WANAFUNZI 3090 WALIOFAULU KWENDA KIDATO CHA KWANZA WAANZA MASOMO YAO

 
WANAFUNZI 3090 wa Wilaya ya Hanang’ katika Mkoa wa Manyara wa shule za msingi waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza kwenye shule za sekondari kwa mwaka 2013 wameanza rasmi masomo yao.
Taarifa hiyo imetolewa na  Mkuu wa wilaya ya Hanang’ Christina Mndeme wakati akiongea  kwenye kikao cha wadau wa elimu wa wilaya hiyo kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili wilayani humo.
Alisisitiza kuwa  wanafunzi hao waliofaulu wameanza masomo yao kwani wilaya yao haina tatizo la ukosefu wa vyumba vya madarasa ya shule za sekondari ambazo wanafunzi hao waliofaulu wamepangiwa.
Alisema kuwa  mwaka 2012 wilaya yao ilishika nafasi ya nne kwa ufaulu kwenye mkoa huo na mwaka 2011 ilishika nafasi ya tatu hivyo mwaka huu wa 2013 wamejipanga washike nafasi ya kwanza kwenye mkoa huo na ngazi ya kanda.
Mkuu wawilayahiyo amewaasa  walimu wa wilaya hiyo kuzifikisha changamoto walizonazo kwa muajiri wao Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo Felix au yeye mkuu wa wilaya hiyo,kuliko kuzipelekwa kwa viongozi wa chama cha walimu (CWT).
“Inashangaza kuwa matatizo yenu mnakuwa mnayafikisha sehemu ambayo siyo husika hivyo mnashindwa kupatiwa msaada mfano mwezi uliopita tulilipa madeni ya walimu 38 na mwezi huu tumelipa madeni 47.Alishangaa mkuu wa wilaya hiyo.
Aidha alisema kuwa  kutokana na kauli mbiu yake ya elimu,kazi na nidhamu zitaondoa umaskini Hanang’ anatarajia walimu,wanafunzi na wadau wote wa elimu wa wilaya hiyo watapandisha kiwango cha ufaulu kwa mwaka huu.
“Tunatakiwa tushirikiane kwa pamoja mimi na ninyi wadau wa elimu na ninyi walimu muache kushiriki migomo isiyokuwa na tija tufanyeni kazi kwa bidii kama kuna tatizo tukae mezani tulijadili na hatimaye tulimalize,” alisema Mndeme.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo