Mwenyekiti wa kamati ya uwasilishaji wa mapendekezo
ya muundo wa mabaraza ya Katiba kwa jamii ya watu wenye ulemavu, Bw.
David Nyendo (kushoto) akiwasilisha maoni yake ya kamati hiyo kwa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba katika mkutano baina yao uliofanyika leo (jumatano
Feb. 13, 2013) katika ofisi za makao makuu ya Tume Jijini Dar es Salaam.
Kulia ni Mjumbe wa Tume, Dkt. Salim Ahmed Salim.
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia)
akizungumza na wawakilishi wa makundi ya jamii ya watu wenye ulemavu
ukiongozwa na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Bw. David Nyendo (kushoto)
mara baada ya kufika katika makao makuu ya Tume leo (jumatano Feb. 13,
2013) kuwasilisha mapendekezo yao juu ya muundo wa mabaraza ya Katiba
kwa jamii ya watu wenye ulemavu. Wa pili kushoto ni Mjumbe wa Tume,
Dkt. Salim Ahmed Salim.