TRA YATOA ELIMU KWA WAFANYABIASHARA

Ofisa Elimu na Huduma kwa mlipa kodi Kanda ya
Mashariki wa Mamlaka ya  Mapato Tanzania (TRA), 

Hamisi Lupenja (kulia), akitoa mada katika semina ya 

siku moja kwa wafanyabiashara wa Kata ya Buguruni 

kuhusu matumizi ya mfumo wa mashine za kodi (EFDs) 

kwa wafanyabiashara wasiosajiliwa na VAT wa 

mkoa wa 

kodi wa Ilala. Semina hiyo imefanyika Dar es Salaam leo. 

(Picha habari na mwaibale.blogspot.com)
Baadhi ya Wafanyabiashara hao wakimsikiliza kwa makini
mwezeshaji wa semina semina hiyo Bw.George Haule.
Wafanyabiashara hao wakimsikiliza kwa makini
mwezeshaji wa semina semina hiyo Bw.Hamisi Lupenja.
Wafanyabiashara hao wakimsikiliza kwa makini
mwezeshaji wa semina  hiyo. Bw.Hamisi Lupenja.
Wafanyabiashara wakiwa katika semina hiyo.
Na Dotto Mwaibale
WAFANYABIASHA nchini wametakiwa kufungua namba ya mlipa kodi (TIN) ili watambulike na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)

Mwito huo umetolewa Dar es Salaam leo na Ofisa wa Elimu na Huduma kwa Mlipa Kodi wa Mkoa wa Kodi wa Wilaya ya Ilala, George Haule wakati akitoa mada katika semina ya siku moja kwa wafanyabiashara wa Kata ya Buguruni kuhusu matumizi ya mfumo wa mashine za kodi (EFDs) kwa wafanyabiashara wasiosajiliwa na VAT wa mkoa wa kodi wa Ilala.

Alisema ni muhimu kwa kila mfanyabiashara kuwa na namba hiyo ya utambuzi kwani itamuwezesha kutambulika na Mamlaka hiyo na itakuwa rahisi kujua kodi anayopaswa kulipa kutokana na biashara yake.

Mwezeshaji mwingine katika semina hiyo Ofisa Elimu na Huduma kwa mlipa kodi Kanda ya Mashariki Hamisi Lupenja  alisema julai 1, 2010 serikali ilianzisha matumizi ya mashine hizo kwa wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa na VAT  lengo likiwa ni kuleta uwiano katika ulipaji wa kodi.

Alisema wafanyabiashara ambao hawajasajiliwa na VAT wataanza kutumia mashine hizo mwaka huu kwa sheria ya kodi ya mapato sura 332 na kanuni ya  mwaka 2012 ndiyo itakayo tumika EFD.

Alisema kutambulika kwa mlipa kodi na kumbukumbu za mauzo yake inaisaidia mamlaka hiyo kujua kupanga kodi kwa mfanyabiashara husika tofauti na kwa mfanyabiashara ambaye hana kumbukumbu.

"Kuweka kumbukumbu za biashara katika kitabu inasaidia hata kwa mtu mwingine kujua mwenendo wa biashara iliyopo hata kama muhusika atakuwa amepata na matitizo ikiwemo kifo" alisema Lupenja.

Wafanyabaiashara hao walisema wamekuwa na changamoto kubwa ya kupangiwa kodi kubwa na mamlaka hiyo jambo linalowafanya washindwe kuendesha biashara zao.

Hata hivyo waliondolewa wasiwasi na Lupenja kwa kuwaambia mamlaka hiyo haimbambikii mfanyabiashara kodi kubwa na akatoa mwito kuwa wawe wazi katika biashara zao.

"Msiwaogope wafanyakazi wa TRA na kuwakwepa kutolipa kodi wanao waogopa ni wale wanaofanyabiashara zao kwa vificho kwani TRA ni rafiki ya ninyi wafanyabiashara" alisema Lupenja


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo