HAPA AKIWA KITUO CHA POLISI UWANJA WA NDEGE JIJINI DAR ES SALAAM
Na Francis Godwin
BAADA ya watanzania wa kada mbali
mbali kutapeliwa kwa njia mbali mbali hasa kupitia mawasiliano ya
simu hatmaye mtuhumiwa mkuu wa vitendo vya utapeli nchini ambae
anamiliki majina zaidi ya matatu kwa kutapelia watu amekamatwa jijini
Dar es Salaam.
Mtuhumiwa huyo ambae anamiliki
majina zaidi ya matano amekuwa akitapeli watu wa kada mbali mbali
wakiwemo wanahabari, walimu na hata wafanyakazi wa Hoteli na watu
wengine wengi leo amekamatwa eneo la Uwanja wa Ndege jijini Dar es
Salaam baada ya mtego kabambe uliowekwa na mmoja kati ya wanawake
waliotapeliwa ambae ni mfanyakazi wa Hoteli moja maarufu jijini Dar es
Salaam (jina limehifadhiwa)
Mfanyakazi huyo wa Hoteli ameueleza
mtandao huu leo kuwa yapata siku
mbili zilizopita tapeli huyo ambae alijitambulisha kwa jina la
Kevin alimpigia simu na kuwa amepata taarifa kutoka kwa mwalimu
wake wa chuo cha Hoteli na utalii kama anatafuta kazi nje ya Hoteli
hiyo hivyo yeye ni meneja wa Hoteli ya Flamingo hivyo yupo tayari
kumpa ajira katika Hoteli hiyo na kama anaowezake kama watano
awaeleze kuwa nafasi ipo.
Imedaiwa kuwa Kevin kama alivyojiita
katika utapeli huo baada ya dakika chache alimpigia tena simu
mwanamke huyo na kumtaka siku ya pili wakutane katika Hoteli hiyo ya
Flamingo ili awaonyeshe mazingira ya Hoteli hiyo na kujua nini cha
kufanya.
Hata hivyo mara baada ya kufika
siku iliyopangwa kama walivyoahidiwa aliwataka kila mmoja kutoa
fedha kiasi cha shilingi 30,000 kwa ajili ya kushonewa sare za Hoteli
hiyo sare ambazo zingekuwa ni mali yao kutokana na wafanyakazi wengi
kuwa na tabia ya kukimbia na sare sasa wameamua kila anayefika
kuomba kazi awe na sare yake toka nyumbani kwake.
Alisema kuwa baada ya kutoka kiasi
hicho cha fedha yeye pamoja na mwenzake mmoja tapeli huyo aliwataka
kukaa nje ya Hoteli hiyo ili afanye mawasiliano na mkurugenzi ndipo
awaite ofisini na baada ya hapo kweli aliingia ofisini ila jinsi
alivyotoka haikufahamika na wao kujikuta wanakaa hadi saa 12 za jioni
bila mtu kuonekana na kuamua kuuliza kwa wahusika na ndipo
walipobaini kutapeliwa baada ya kuambiwa hakuna ajira mpya
zilizotangazwa hapo na kuwapa utaratibu wa ajira unavyotumika
kutangazwa katika Hoteli hiyo.
Kutokana na kulizwa kiasi hicho cha
pesa kitu cha 60,000 kwa wawili ndipo usiku alipompigia simu tapeli
huyo na kujifanya akiulizia majibu kwa madai kuwa jana alipatwa na
msiba hivyo aliondoka mapema zaidi .
"Kweli baada ya kumpigia simu tapeli
alionekana kuwa mkali zaidi kuwa ni mambo gani nimefanya yeye
alitoka kujua kutufuata hakukututa hivyo akataka kujua lini
nitakuwa tayari kufika ili nianze kazi...na ndipo nilipomwomba nafasi
yangu nimpe mtu mwingine mimi nilidanganya kuwa nitachelewa kurudi
....ila bila kujua nilikuwa namtega alikubali na kusema nimpe namba za
huyoa atakayechukua nafasi yangu na wengine wawili kama wapo...na
hapo ndipo nilipoweka mtego na leo tumemkamata"
Tapeli huyo amekuwa akijiita majina mbali mbali likiwemo la Abdalah Mkwachu, Aman kwa namba hizi 0713094986,07162404425
Pia inadaiwa ndie aliyepata kutapeli watu kupitia ajira hewa za TGNP kwa kutumia jina la Lilian Dihalo, mwenye
namba za simu 0717-196386 ila pia inasadikika ndie aliyewaliza
wanahabari wengi nchini kupitia jina la Zuhura Kambangwa.
Mbali ya makundi hayo tapeli huyo
anadaiwa kuwatapeli walimu na watu mbali mbali maarufu nchini kwa
sasa anashikiliwa na jeshi la polisi.