
Na Ibrahim Yassin,Kyela
MWENYEKITI wa baraza la madiwani katika halmashauri ya wilaya Kyela ,Gagriel Kipija aliesema
kuwa ipo haja sasa kwa serikali kuu kwa kuziheshimu hamashauri hapa nchini
kuliko ilivyo sasa
Alisema kuwa
halmashauri nyingi hazitendewi haki na serikali kwa mambo mengi kiasi cha
kukwamisha shughuli za maendeleo na kuwapa wakati mgumu madiwani kujieleza pale
wanapohojiwa na wananchi wao pale wanapoona miradi mingi inasinzia
Kauli hiyo
ameitoa jana kwenye kikao cha dharura cha baraza la madiwani ambao waliagizwa na
serikali kuu kupitisha bajeti haraka kabla ya kikao cha bunge kuanza na kupitisha bajeti ya
Tshs,23,437,095,997,00 kutoka katika
vyanzo mbalimbali vya mapato
Mwenyekiti
huyo wa halmashauri alisema kuwa wamekuwa wakipanga bajeti zao kwa kutegemeana
na ruzuku kutoka serikali kuu cha ajabu fedha za serikali kuu zimekuwa hazifiki
katika hamashauri na kama zikifika hazifiki kwa wakati kiasi cha kukwamisha
shughuli za maendeleo
Alisema
kitendo hicho cha serikali kushindwa kupeleka fedha katika halmashauri ni
kitendo cha dharau ambacho serikali inabidi kujisahisha na hari ikiendelea
hivyo wao hawataendelea kupitisha bajeti ambazo mwisho wake jamii itawaona kuwa
ni waongo kwa baadhi ya miradi kushindwa kutekelezeka kwa wakati au kushindwa kutekelezeka kabisa baada
ya
kukosekana kwa fedha ambazo serikali kuu haizipeleki kwenye halmashauri
Katika
baraza hilo pia madiwani hao walitaka bajeti hii ya 2013/14 iweze kushughulikia
baadhi ya kero nyingi ambazo zimedumu kwa muda mrefu bila ya kuzishughulikia
Diwani wa
kata ya Busale Ezekiel Msyani alisema kuwa moja ya kero kubwa na ambayo imedumu
kwa muda mrefu ni tatizo la maji na kuiomba serikali katika bajeti hii mpya
kuhakikisha kuwa wanaiangalia kwa umakini kero ya maji na kulazimika kutumia
baadhi ya fedha katika mapato ya ndani kuyalazimisha kwenda kushughulikia
tatizo hilo la maji
Mkurugenzi
mtendaji wa halmashauri ya wilaya Abdallah Mfaume kwa upande wake alisema kuwa tatizo la halmashauri kutopata
fedha kutoka serikali kuu ni la kitaifa na kuwa hivi sasa fedha zitakuja na
miradi yote itatekelezeka vizuri
Mkuu wa
wilaya Kyela Magreth Malenga alisema kuwa hari hiyo ya serikali kutoleta fedha
kwa wakati ni moja ya mambo yaliyofanya halmashauri kushindwa kutekeleza
majukumu yake ipasavyo
Na aliwaomba
madiwani hao kuwa wavumilivu kwa serikali iliyopo madarakani kwani hivi sasa
serikali ina fedha za kutosha za kuweza
kutatua kero mbalimbali zilizopo katika kata zao