Na Ibrahim Yassin, Kyela
WANACHAMA wa chama cha Mapinduzi (CCM)wilayani Kyela mkoani
Mbeya wapo hatarini kupata magonjwa ya milipuko kutokana na kukosa huduma ya
choo kwa muda wa zaidi ya miaka 15 katika ofisi ya chama wilaya,ali inayo
walazimu baadhi ya wanachama kujisaidia
katika vyoo vilivyopo kwenye nyumba za jirani na ofisi hiyo.
Kukosekana kwa huduma hiyo ya choo kwa muda mrefu kuna
shusha hadhi ya chama hicho kutokana na ukubwa wake na kimekuwa kikipata haibu
kubwa hasa pale wanapofika wageni kutoka mikoani ambao wanafika ofisini hapo
kwa shughuri za kichama wanapelekwa kujisaidia katika vyoo vilivyopo jirani na
ofisa hiyo pindi wanapo hitaji huduma ya choo.
Akitoa majibu kwa waandishi wa habari kuhusu tatizo hilo
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi
walayani Kyela Dkt Hanta Mwakifuna,mbali na kukiri kuwepo na tatizo hilo
alisema kuwa yeye kama mwenyekiti amechukua jukumu hilo la kuanza mchakato wa
ujenzi ili kuodoa kero inayoipa kashfa
ofisi yake.
Alisema kuwa ofisi yake imetenga kiasi cha tsh,7000,000/ = kwa
ajili ya kuanza kuondoa tatizo hili kwa kuweka mipango ya muda mfupi na kwamba
wameunda kamati ndogo ya ujenzi yenye wajumbe 6 wakiongozwa na wajumbe 2 wa
kamati ya siasa ambapo kazi hiyo ya
ujenzi itakamilika ndani ya siku 90.
Dkt ,Mwakifuna ambaye pia ni diwani wa kata ya Ipinda
aliwataja viongozi wengine waliopo kwenye mchakato huo kuwa ni mkuu wa wilaya
Magreti malenga (Mwenyekiti)Mwenyekiti wa haimashauri Gabriel Kipija( makamu)na Patrick Mwampeta (mtunza
hazina)ambapo wamekubaliana kila diwani atoe Tsh,90,000 na kila mjumbe wa
kamati ya siasa ya wilaya atatoa
Tsh,30,000/-ambao kwa idadi yao watafikisha kiasi hicho cha 7000,000/kitakacho
kamilisha ujenzi huo ndani ya siku 90.
Sambamba na hilo
mwandishi wa habari hizi alihoji kuhusu ujenzi wa ofisi ya chama kwamtindo wa
ghorofa ulioahidiwa kujengwa na mbunge wa jimbo la Kyela wakati akiomba ridhaa ya kuwa mbunge kwa wanachama,na wanachama hao
walimpa nafasi ya kuwa mbunge lakini amemaliza miaka 8 tangu awe mbunge na
hakuna dalili ya kuwepo na ujenzi huo,na kibaya zaidi hata choo tu hakuna.
Akijibu hoja hiyo mwenyekiti mwakifuna,alidai kuwa ni kweli
mbunge aliahidi lakini ujenzi huo wa ofisi ya chama kwa mtindo wa ghorofa
haujaanza ,na kuwa yeye alipochaguliwa kuwa mwenyekiti alimkumbusha mbunge juu ya kuanza kwa ujenzi
huo ambapo mbunge alimuahidi kuwa ujenzi huo utaanza muda si mrefu .
“Nilipochaguliwa mwenyekiti
wa chama wilaya nilimkumbusha mbunge juu ya ujenzi wa ofisi hiyo kwa
mtindo wa ghorofa na mbunge amelipokea na tayali amenipa ramani kilichobakia ni
michakato midogo midogo ikikamilika ujenzi huo utaanza”,alisema Dkt Mwakifuna.
Dkt Mwakifuna alimaliza kwa kuwataka wanachama wa chama cha mapinduzi kuwa na mshikamano na
uvumilivu katika kukijenga chama hasa kipindi hiki wanapoelekea kwenye uchaguzi
wa wenyeviti wa vijiji na vitongoji ili wananchi wawe na imani na chama hicho
na kuendelea kukipa ridhaa ya kuendelea kuongoza nchi.
