Rais Dkt.Jakaya Kikwete akimpa pole Rais Yoweri Kaguta Museveni
kutokana na kifo cha Baba yake Mzee Amos Kaguta, katika kijiji cha
Rwakitura nchini humo.
Rais Dkt.Jakaya Kikwete akifariji mke wa Rais wa Uganda Mama Janet
Museveni kufuatia kifo cha Baba wa Rais Museveni Mzee Amos Kaguta.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiweka shada la maua juu ya jeneza la
Marehemu Mzee Amos Kaguta(97),Baba Mzazi wa Rais Wa Uganda Yoweri Kaguta
Museveni wakati wa ibada ya mazishi iliyofanyika katika kijiji Cha
Rwakitura nchini Uganda.
Rais Dkt. Jakaya Kikwete na mwenyeji wake Rais Yoweri Kaguta Museveni wa
Uganda wakiweka udongo kwenye kaburi la Mzee Amos Kaguta(97) wakati wa
mazishi yake yaliyofanyika katika kijiji cha Rwakitura. PICHA ZOTE NA
FREDDY MARO, IKULU