WAMCHOMA MWENZAO NDANI YA NYUMBA KISA UGOMVI WA ARDHI




Mkazi wa Kijiji cha Ochuna Kata ya Nyathorogo tarafa ya Luo Imbo Wilayani Rorya Mkoani Mara ,Samson Jeremia (49) amefariki dunia baada ya kuchomewa ndani ya nyumba yake usiku na watu wanaosadikiwa kuwa na ugomvi naye kuhusu ardhi.

Katika tukio hilo Prisca Samson (35) ambaye ni mke wa marehemu,alinusurika kwa kuokolewa na majirani akiwa hoi baada ya kuvunja milango ambapo kwa sasa amelazwa katika Hospitali ya Kowak Wilayani Rorya akiwa na majeraha ya kuungua kwa moto mwili mzima.

Kamanda wa Polisi Tarime-Rorya, Kamishina Msaidizi Justus Kamugisha alisema leo kuwa  tukio hilo limetokea  jana, Februari 23 Usiku nyumbani kwa Samson Jeremia, ambapo ilidaiwa kundi la Watu wanaosadikiwa kuwa na uhasama wa kugombea mashamba walifika na kufanya uhalifu huo wa kuchoma nyumba wakati Samson akiwa amelala na mke wake Prisca.

Alisema, watu hao walifunga milango kwa nje ili wasiweze kutoka nje wauungulie ndani wote, lakini moto ulipokolea mke alipiga Kelele za kuomba msaada huku moshi ukiwa umejaa ndani ya nyumba.

Kamanda Kamugisha alisema kuwa  polisi wamewakamata watu wawili kuhusiana na tukio hilo na kuwataja kuwa ni  Silveri  Abela Anundu (75) na ndugu yake Ezekia Kachula Anundu ( 80) na kwamba polisi waendelea na msako wa kuwapata wengine waliohusika katika Tukio.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo