MADIWANI WATILIWA SHAKA KUWEPO KWENYE MABARAZA YA KATIBA

Jukwaa la Katiba nchini limepinga ushiriki wa madiwani katika mabaraza ya katiba yanayotarajiwa kuundwa na kubainisha kuwa diwani anayetaka kushiriki anapaswa kugombee nafasi hiyo kama ilivyo kwa watu wengine.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam Mwenyekiti wa Jukwaa la Katiba DEUS KIBAMBA amesema iwapo madiwani watashiriki katika mabaraza hayo wataingiza siasa na kuharibu mchakato wa kazi za mabara kwani wao ndiyo wasimamizi wa mikutano yak kata yenye jukumu la kuchagua wagombea.

Pamoja na kuwakataa madiwani pia KIBAMBA amesema kigezo cha raia wa Tanzania ndiye anapaswa kushiriki kwenye mabara hakitoshi kutokana na kuwepo kwa aina nyingi za Raia hivyo ni vema kiainishe kuwa raia mzawa ili kupata watu wazalendo na wenye uchungu na nchi.

Katika hatua nyingine KIBAMBA ameipongeza Tume yak Katiba kwa kutoa muongozo kabla yak kuundwa kwa mabaraza na kupendekeza utaratibu huo uendelee kutumika katika hatua zote muhimu za kutafuta katiba ya nchi.

Kwa mujibu wa muongozo uliotolewa na Tume yak Katiba jumla yak watanzania Elfu 19 mia tatu sitini na saba watashiriki huku Baraza la Katiba nalo likiahidi kuunda mabaraza yatakayochukua watu wengi zaidi kupitia asasi za kiraia ili kupanua wigo wa kukusanya maoni na kuboresha katiba.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo