MADIWANI MAKETE WAANZA KUJADILI MAENDELEO YA WILAYA YAO


Baraza la madiwani halmashauri ya  wilaya Makete limeanza kujadili utekelezaji wa shughuli za kimaendeleo katika ngazi ya kata ,kwa mwaka wa fedha 2012/13 wilayani hapa

Akifungua baraza hilo mwenyekiti wa madiwani Mh.Danieli Okoka amesema kuwa kila diwani anawajibu wa kuandaa na kutoa taarifa kwa wananchi wake

Kwa upande wa mwakilishi wa kata ya Tandala diwani wa Lupalilo Mh Manase amesema kuwa kata hiyo inakabiliwa na upungufu wa watumishi kama wenye viti wa vijiji vya Ihela na Ikonda ,Bibi afya pamoja na mtendaji wa  kata ya ikonda

Aida diwani wa kata ya Itundu Mh. Mwinuka amesema kuwa kata yake inakabiliwa na upungufu wa pembejeo za kilimo ikiwemo mbolea za kupandia na kukuzia

Jumla ya kata 22 kupitia madiwani wamewakilisha taarifa za utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa mwaka wa fedha  2012/2013, Huku changamoto kubwa ikiwa ni upungufu wa watendaji wa kata na vijiji 


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo