CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Makao Makuu kimepinga maamuzi ya Kamati ya Utendaji ya Chama hicho Wilaya ya Musoma cha kuwavua Uanachama madiwani wawili wa viti maalum Habiba Ally Zeddy na Mariam Daudi Chacha na hivyo kupoteza sifa ya kuwa madiwani kwa mujibu wa Katiba ya Chama hicho.
Katika barua iliyotumwa na Afisa Sheria wa Chama hicho Ester Daffi yenye kumbukumbu namba C/HQ/M/MARA/10/101 ya tarehe 22/2/2013 kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Chama hicho Willbord Slaa ilisema kama kuna utovu wa nidhamu kwa wahusika ilitakiwa kuzingatia masharti ya Katiba na Kanuni hasa kanuni ya Uendeshaji kazi za Chama ibara ya 6.5.2 pamoja na Kanuni ya 8.0 (a) na (b) ya nidhamu kwa madiwani.
Katika barua hiyo ilidai suala hilo lilitakiwa kutolewa taarifa Makao Makuu kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye Kamati Kuu kwa ajili ya maamuzi kwa kuwa mamlaka ya kuwavua Uanachama yanapaswa kuzingatia kanuni tajwa ya katiba ya Chama hicho.
Alisema Makao Makuu ya Chama hicho imepinga maamuzi hayo kutokana na madiwani hao kukata rufaa kupinga maamuzi hayo katika barua yao ya rufaa iliyotumwa kwa njia ya nukushi tarehe 21/2/2013 na kuipitia kwa kina na kisha kutoa maamuzi hayo kwa mujibu wa katiba.
Ilidaiwa katika barua hiyo ambayo nakala yake imepelekwa kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma ilisema kamati ya Utendaji ya Chadema Wilaya ya Musoma haikuzingatia barua kutoka Ofisi ya Katibu Mkuu wa Chama hicho ya tarehe 16/2/2013 yenye kumbukumbu namba C/HQ/M/MARA/101.
Katika barua hiyo iliyokuwa na kichwa cha Habari (MGOGORO NDANI YA HALIMASHAURI YA MANISPAA YA MUSOMA) ilidai tarehe 15/2/2013 Mkao Makuu ilipokea taarifa kutoka kwa Mstahiki Meya wa Manispaa ya Musoma Alex Kisurura kuhusu mgogoro unaoendelea ndani ya ya Halimashauri hiyo ukihusisha baadhi ya Viongozi wa Chama wa Jimbo.
Katika barua hiyo ilidai Halimashauri ya Manispaa ya Musoma inaongozwa na (CHADEMA) na kwa mujibu wa kanuni ibara ya 3.1 (a) (c) (g) na (i) ya kanuni za kusimamia Shughuli,Mwenendo na Maadili ya Halimashauri zilizo chini ya Chadema,Ofisi ya Katibu Mkuu kwa azimio la Kamati Kuu ndiyo msimamizi wa shughuli za Halimashauri za Chadema Nchini.
Barua hiyo ilida Agenda kuhusu mgogoro ndani ya Halimashauri au kutofautiana kwa Meya na madiwani na au Uongozi wa Chama isijadiliwe mpaka mchakato wa ndani ya Chama utakapokamilika au kwa maelezo kutoka Makao Makuu na pindi itakapokwenda kinyume hatua za kinidhamu kwa mujibu wa Katiba na Kanuni za Uendeshaji Kazi za Chama zitachukuliwa dhidi ya wote watakaokiuka maelezo yaliyotolewa.
Akizungumza na blog hii mara baada ya kupokea barua ya majibu ya rufaa kutoka Mkao Makuu ya Chadema,Diwani Habiba Ally Zeddy alisema licha kushinda rufaa yao ya kuvuliwa Uanachama Makao Makuu inapaswa kuangalia kwa karibu mwenendo wa Chama hicho Wilaya ya Musoma.
Alisema maamuzi ya kuvuliwa Uanachama waliyofanya Kamati ya Utendaji na kutangazwa katika Vyombo vya Habari ni kama wamezalilishwa kwani hadi sasa licha kutolewa maamuzi ya kuvuliwa hakuna barua yoyote waliyopewa kuhusu kuvuliwa Uanachama na kukosa sifa ya kuwa madiwani.
SOURCE:SHOM MMBINDA