Jeshi la polisi
mkoani Mwanza linamshikilia Imamu mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la
Hamza mkazi wa jijini humo kwa kosa moja la utengenezaji wa CD zenye uchochezi
wa kidini ambazo zimekuwa zikisambazwa katika mitaa na misikiti ya jijini
Mwanza
Akizungumza jijini
humo kamanda wa polisi mkoani Mwanza Ernest Mangu amesema Imamu Hamza
amekamatwa katika oparesheni ya kutafuta watu wanaodaiwa kuchochea chuki za
kidini
Mbali na Imam Hamza
kukamatwa pia jeshi hilo linamtafuta sheikh
Ilunga Hasan Katanga
na Mkurugenzi wa kituo cha redio cha Kwa neema FM Askofu Augustino Mpemba
ambaye kituo chake kimefungiwa kwa uchochezi nao wanatuhumiwa kutengeneza kanda
za uchochezi baina ya wakristo na waislamu na kuzisambaza
Msikilize kamanda
Mangu akizungumzia suala hilo