Jaji
Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga (katikati) akibadishana mawazo na
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Joseph Warioba (kulia)
na Mjumbe wa Tume, Dkt. Sengondo Mvungi nje ya ukumbi wa Tume Jijini Dar
es Salaam mara baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa
Tume leo Ijumaa (Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga alikutana na Wajumbe ili
kubadilishana mawazo na uzoefu katika uandishi wa Katiba Mpya.
Makamu
Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba, Jaji Mkuu mstaafu
Augustino Ramadhani (kushoto) akibadilishana mawazo na Jaji Mkuu wa
Kenya, Mhe. Willy Mutunga nje ya ofisi za Tume Jijini Dar es Salaam mara
baada ya kumalizika kwa mkutano kati yake na Wajumbe wa Tume leo
(Ijumaa Feb. 15, 2013). Mhe. Mutunga amekutana na Wajumbe wa Tume
kubadilishana mawazo na uzoefu wake kuhusu uandishi wa Katiba Mpya.
Mjumbe wa Tume
ya Mabadiliko ya Katiba, Prof. Palamagamba Kabudi (kushoto)
akimwonyesha nakala ya Kitabu Jaji Mkuu wa Kenya, Mhe. Willy Mutunga
(katikati) nje ya ofisi za Tume mara baada ya kumalizika kwa mkutano
kati yake na wajumbe wa Tume baina yao uliofanyika katika ofisi za Tume
Jijini Dar es Salaam leo (Ijumaa Feb. 15, 2013). Mhe. Mtungi amekutana
na Wajumbe wa Tume kuzungumzia uzoefu wake kuhusu uandishi na
utekelezaji wa Katiba Mpya. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume, Jaji Joseph
Warioba. (PICHA NA TUME YA KATIBA)
