Bw.
Raymond Francis mratibu wa zoezi hilo, na mtangazaji wa kituo cha Radio
Ebony fm akitoa nasaha juu ya harambee na siku ya Wapendanao- VALENTINE
DAY, katika hafla ya kukabidhi misaada kwa watoto yatima.
WAKATI akili, Mioyo na fikra za
wananchi walio wengi duniani kote zikielekezwa katika siku ya wapendanao
almaarufu kama “VALENTINE DAY” kama ni siku ya kimahaba na kimapenzi, mambo hayo yamekuwa tofauti kwa wakazi wa
mikoa ya nyanda za juu kusini- Iringa, Mbeya..
Hatua hiyo imekuja baada ya radio
Ebony fm iliyopo katika mkoa wa Iringa kubadili mfumo na utaratibu huo, na
hivyo kuwahamasisha wananchi kuchangia ili kuwatembelea kundi la watu wenye
mahitaji muhimu.
Akizungumzia mpango huo, mratibu wa
zoezi la hilo lenye kaulimbinu ya “VALENTINE
DAY 2013, UPENDO KWA WATOTO” kupitia kampuni ya Ebony fm, Bw. Reymond Fransis Chali
- amesema lengo la kuendesha harambee hiyo ni kuwakumbuka watu wenye mahitaji
muhimu ambao wamesahaulika katika jamii, hasa katika siku hiyo ya wapendanao.
“Imezoeleka kama siku hii ya
VALENTINE ni malumu kwa wapenzi, katika kununuliana kadi, Maua mekundu, na
zawadi mbalimbali, fikra hizi kupitia kituo chetu cha Ebony nikaamua kubadili
mawazo hayo na hivyo kuwaelekeza wananchi kuwakumbuka watoto yatima na wale
wanaoishi katika maisha magumu na hatarishi,” Amesema Reymond.
Aidha Reymond amesema anawashukuru
wananchi wote waliopokea kwa mikono miwili zoezi hilo na kwa kuitikia harambee
hiyo ya uchangiaji wa fedha na mahitaji mbalimbali kwa watoto wa kituo cha “SISI
NI KESHO” kilichopo kijiji cha Nyololo katika Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa.
Amesema jumla ya fedha
zilizochangwa na wananchi kupitia M-PESA ni zaidi ya shilingi Milioni 9.5, huku
baadhi ya wananchi wakijitolea kwa hali na mali vifa mbalimbali kama Magodoro
zaidi ya 15, nguo, mashuka, Mablanketi, Viatu, Vinywaji baridi (Visivyo na
kileo), Katoni za Sabuni, Sukari, Unga wa ugali na Ngano, madishi ya kufulia na
kuogea na hata mabero ya nguo mbalimbali.
Ofisa tawala wa Wilya ya Mufindi Bi.
Maria Waitara ameitaka jamii kuiga mfano huo, kwa kuyakumbuka makundi hayo,
hasa hilo la watoto yatima ambao kwa kiwango kikubwa wamepoteza wazazi wao kwa
tatizo la ugonjwa wa ukimwi.
“Kwa kweli Radio Ebony imetupa
somo, kubadili sura ya siku ya VALENTINE kwa kuwakumbuka watoto hawa,
tunatakiwa kuendeleza zoezi hili ambalo katika wilaya yetu limetusaidia, kwani
watoto hawa ni wetu wote, kuna watu watu wanafanya maasi mengi katika siku kama
hii, lakini hawa ndugu zetu wameamua kuleta misaada hii ambayo itawasaidia kwa
muda mrefu watoto wetu,” Alisema Waitara.
Hata hivyo Bi. Suzana Mfugale mmoja
wa wahudumu wa kituo hicho cha “SISI NI KESHO” akisoma lisara katika hafla hiyo amesema changamoto
inayokikabiri kituo hicho ni pamoja na jamii kutojihusisha katika kuhudumia
watoto hao, na hivyo kuwepo kwa mapungufu mengi.
source:Olivermoto blog