Makamu Mwenyekiti wa Chadema Taifa
Said Arfi, akihutumia katika mkutano wa hadhara wa Dodoma kwenye
Viwanja vya Mwanga Bar na kuhudhuliwa na umati wa watu.
Na Bryceson Mathias-Dodoma.
MAKAMU
Mwenyekiti wa chama cha Demokrasi na Maendeleo Taifa na Mbunge wa
Mpanda Mjini, Said Arfi, amewataka watanzania kamwe wasikubali
kugawanywa, kudanganywa, kutenganishwa na kukosanishwa na Chama cha
Mapinduzi (CCM) kinachopandikiza itikadi za udini.
Arfi
alisema hayo katika Mkutano wa adhara uliofanyika katika Viwanja vya
Mwanga Bar mkoani Dodoma Akihutubia maelfu ya watu ambao baadaye
walijipanga na kuwapa kadi za Chadema baada ya kuamua kuvua Magamba na
kuvaa Magwanda Arfi alisema, awali CCM walitumia njia hiyo kwa kukiita
Chama cha wanachi CUF ni cha Ki-Islam na wakafanikiwa kukisambaratisha
kwa Wakristo kukihama.
“Baada
ya Mbinu za kukiita Chadema ni kikabila na kwamba ni cha Kikristo
kushindwa, sasa wameanza kutafuta Mbinu za kuwapotosha, kuwadanganya,
ili kuwatenganisha, kuwakosanisha, kuwaogofya, kuwatishia na
kuwapandikizia udini”.alisema Arfi akisema yeye ni M-Islamu na hajawahi
kupata hasara.
Huku
akishangiliwa na uwanja mzima Arfi alisema, yeye ni M-Islamu, hakuna
mahali ndani ya Kurani panaposema mtu aue halafu Mungu atampa kheri na
pepo, akiwa Ahera zaidi ya Laana kumuanzia hapa duniani.
Aliwashukia
Polisi na Usalama wa Taifa kuwa ifike mahali wasione aibu kusema
wameshindwa wajibu wao wa kuwalinda watanzania, jamboa alilosema kama
wameshindwa, sasa wanatakiwa wakae pembeni na
wakikaidi watalazimishwashwa na guvu ya Umma.
Mbali
ya shutuma hizo Arfi aliitaka Serikali ya CCM iwaombe radhi watanzania
kwa kuwaigiza kwenye ugomvi wa kidini, ambapo hapo awali alisema hakuna
mtu aliekuwa akiuliza habari ya kuchinja na kugombea madarakani kwa
Udini, Ukabila, Undugu, Urafiki na Upenzi.
Arfi
aliiponda CCM na Viongozi wake akisema, hivi sasa wanatumika kupoteza
fedha za walalhoi mamilioni kwa mamilioni kupigia kura ya maajabu ya
Mlima Kilimanjaro, Hifadhi ya Ngorongoro na Hifadhi ya Serengeti, badala
ya kutumia fedha hiyo kukomesha maajabu ya mtoto kufaulu mtihani kwenda
Sekondari wakati hajui kusoma, kuandika na kuhesabu.
Aidha
aliwasihi watanzania wajiulize mioyoni mwao, Je kura yao imewasaidia
nini? Kama haijawasaidia basi kwa mtu yeyote waliyempa madaraka na
wajibu huo, basi waihukumu Serikali hiyo mwaka 2015 na kudai hilo
litawezekana tu kwa kuunganisha nguvu na kuing’oa CCM madarakani.
Awali
Kigaila akiwahutubia wana Dodoma kabla ya kumuachia Uwanja Arfi alisema,
Kitendo cha Spika wa Bunge Anne Makinda kuzima Hoja za Wapinzani ya
James Mbatia kuhusu Udhaifu wa Sekta ya Elimu yenye Maslahi kwa
Watanzania na ya John Mnyika kuhusu Shida ya Majiji Jijini Dar es Salaam
na nchi nzima, ingekuwa ni Arusha asingeingia bungeni wananchi
wangemzuia kwa nguvu ya umma.
Huku
akishangazwa na uoga wa wananchi hao, Kigaila aliwashukia akisema,
wakazi wa Dodoma ikifika hapo ndipo mahali huwa wanauza utu na kupoteza
haki yao ambapo watu hurudi nyuma na kujificha kwenye uchochoro wa
nyumba na Mitaa yao wakajifungia ndani.