Na Willy Sumia, Katavi
JESHI la polisi mkoani Katavi limetakiwa kubadili utendaji kazi wake
ili kujenga imani ya ushirikiano baina ya jeshi hilo na wananchi
katika juhudi za kuutokomeza uhalifu mkoani humo
Hayo yalibainishwa jana na wananchi wa kata ya Kawajense katika
mkutano wa hadhara wa polisi jamii uliofanyika katika eneo la Bar ya
Web Site iliyoko jirani na shule ya msingi Nyerere katika kata hiyo
mjini Mpanda ambapo Kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Katavi alikuwa
akitoa elimu ya polisi jamii kwa wananchi
Wananchi hao walilalamikia vitendo vya baadhi ya askari wa jeshi hilo
kutoa siri ya watoa taarifa kwa wahalifu na hivyo kujenga chuki na
kuhatarisha usalama wa watoa taarifa na hivyo kudhoofisha juhudi za
kupambana na uhalifu mkoani humo.
Wakizungumza wananchi hao waliwasihi viongozi wa jeshi hilo ngazi ya
wilaya kuiga utendaji kazi wa aliyekuwa mkuu wa polisi wa wilaya hiyo
na baadaye kupelekwa mkoani kuwa aliweza kupambana na uhalifu hadi
akafanikiwa kuondoa wimbi la ujambazi lililokuwa limeota mizizi
wilayani Mpanda.
Akizungumza katika mkutano huo kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa
Katavi, Dhahiri Kidavashari aliwasihi wananchi kutokukata tamaa kwa
changamoto ndogo ambazo zinaweza kutatuliwa na yeye mwenyewe tena kwa
muda mfupi sana, wanachopaswa kufanya kuanzia sasa ni kumpa taarifa ni
askari gani anafanya huo mchezo mchafu wa kiuaji.
Alisema anachoomba kwa wananchi ni kumpa taarifa kwa njia ya simu kwa
namba alizozitoa au kumuona popote watakapokutana naye kuhusu matukio
ya kuvujisha siri wanazotoa kwa jeshi la polisi ili aweze kuchukua
hatua haraka na kwa wakati ili Katavi iendelee kuwa salama bila
majambazi.