Mratibu msaidizi wa kudhibiti ukimwi mkoa wa Iringa akizungumza na
waandishi wa habari kuhusu mikakati ya kudhibiti ukimwi na matumizi ya
ukimwi
naibu meya wa manispaa ya Iringa Gervas Ndaki akifungua mdahalo wa
kudhibiti ukimwi na matumizi ya madawa ya kulevya
mmoja wa wanafunzi Neema Magoma akichangia mada katika mkutano huo
Halmashauri ya Manispaa ya Mkoa wa Iringa imeandaa mikakati thabiti ya
namna ya kupambana na kuzuia maambukizi na matumizi ya dawa za
kulevya yanayozidi kuongezeka kwa kasi mkoani hapa.
Mwandishi Denis Mlowe
anaripoti kuwa hayo
yamesemwa na Msaidizi wa Kudhibiti maambukizi ya virus vya ukimwi
Gasper Nsanye wakati wa mdahalo ulioandaliwa na AMMICAL wa mpango wa
majadiliano ya viongozi na wadau mbalimbali ulifanyika katika ukumbi wa
hallfare na kuwashirikisha rika mbalimbali wakiwamo wanafunzi wa vyuo
vikuu, sekondari na shule ya msingi na kufaidisha mkoa wa Iringa na
wilaya za Temeke, Kinondoni na Ilala za Dar es Salaam.
Amesema kwamba mkoa wa Iringa umekumbwa na makundi matatu ambayo
yamesaulika katika jamii kuhusiana na maambukizi ya
ukimwi na na matumizi ya madawa ya kulevya na ndio chanzo cha kuenea
kwa kasi kubwa katika manispaa na kuifanya kuwa ya kwanza kitaifa kwa
maambukizi ya ukimwi.“Lengo la kufanya mdahalo huu ni juu
ya athari za dawa za kulevya na ukimwi kuzuia na kudhibiti kabisa hadi
kufikia hatua ya sufuri 3 katika kuenea kwa ukimwi, unyanyapaa na
biashara ya madanguro na vijana wanaotumia madawa ya kulevya kufikia
hatua ya sifuri 3” alisema Nsanye
Aidha amesema kwamba mkoa wa Iringa ni wa kwanza kitaifa ukiwa na
asilimia 15.7 hivyo lengo pia
ni kuweka mikakati ya namna ya kukabiliana na vvu na ukimwi ili
kupunguza vifo kufikia sifuri na kusaidia makundi hayo matatu ambayo ni
baishara ya ngono,wanaojidunga madawa ya kulevya na wanaume wanaofanya
mapenzi ya jinsi moja(ushoga).
Awali
Naibu Meya wa Manispaa ya Iringa Gervas Ndaki amesema kwamba kwa sasa
Iringa imeingiliwa na makundi hayo na ndio chanzo kikubwa cha kuenea kwa
maambukizi katika manispaa na ni jukumu la kitu mwananchi kuweza
kupambana na makundi haya kwa kuwapa elimu na kuweza kuwasaidia
kuondokana na tabia hatarishi. “ Ni lazima tutokomeze haya makundi na
jamii
yatakiwa kutambua kwamba makundi haya yapo na yanasababisha maambukiz
makubwa ya virus vya ukimwi katika mkoa wa Iringa” amesema Ndaki.
Naye mwenzeshaji Dr
Jayson Mboya amesema kwamba kwa sasa watu milioni 33.3 wanaishi na
virus vya ukimwi na wengi wao wako Kusini mwa Jangwa la Sahara ikiwemo
Tanzania yenye watu milioni 1.6 na chanzo kikubwa ni
ngoni zembe zikiambatana na tabia hatarishi kama kujidunga madawa ya
kulevya kwa kuazimana sindano, unywaji wa pombe kupita kiasi na wafungwa
wanaofanya mapenzi ya jinsia moja.
Amesema jamii yatakiwa kuelimishwa kwa kiasi kikubwa madhara na athari
ya utumiaji wa madawa ya kulevya waweze kujiepusha na kutotumia kabisa
aidha kuongezwa kwa vituo vya afya vitakavyohudumia waathirika wa
madawa kulevya na vijana kujishughulisha na shughuli mbalimbali
zikiwemo michezo.