NDEGE YA ATCL YAANZA SAFARI BAADA YA MATENGENEZO

ATCL 1
Marubani   wa Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) wakiwa wanafanya ukaguzi wa mwisho kabla ya kuanza safari ya kutoka Kigoma kuenda Dar es Salaam leo asubuhi. Hii ni baada ya wahandisi wa shirika hilo kukamilisha kufunga kioo kipya ambacho kimenunuliwa kutoka nchini Marekani. Ndege hii aina ya Dash-8 Q300 yenye namba za usajili SH-MWF ambayo ilisitisha safari zake za Kigoma baada ya kioo cha mbele katika chumba cha marubani kupata ufa (Wind shield crack) tarehe 11 Januari, 2013, muda mfupi baada ya
ndege hiyo kuruka kutoka Kigoma kurudi Dar Es Salaam katika safari zake za kawaida, imeanza tena safari za Dar-Kigoma-Dar kulingana na ratiba .
ATCL 2Kapteni  Maqbool Sange akiwa ndani ya chumba cha marubani akifanya ukaguzi wa mwisho wa ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya Dash-8 Q300 .
Ndege hiyo leo imetua katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere ikitokea Kigoma ikiwa imebeba abiria 22.
Uongozi wa Shirika imedhibitisha kuwa safari za Dar-Kigoma-Dar zitaendelea kama ratiba inavyosema.
ATCL 3 
Abiria wakipanda ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) katika uwanja wa ndege wa Kigoma, tayari kwa safari ya kuelekea Dar es Salaam.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo