WAGONJWA WA KIPINDUPINDU WALAZWA CHINI YA MTI

Mgonjwa wa Kipindupindu akiwa amelazwa chini ya mti katika kambi ya Muze
Mhudumu wa kambi ya wagonjwa wa Kipindupindu akitoa huduma chini ya mti
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga ambaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kalamo Moshi Chang'a akiwa akiwahoji wahudu wa kituo hicho kutokana na mazingira machafu na kukosekana kwa huduma muhimu kwa wagonjwa hao
Mkuu wa wilaya Moshi Chang'a akiwa na Mbunge wa Kwela Ignas Malocha mwenye suti nyeupe (katikati) wakimhoji Afisa Afya wa kata ya Muze

Mkuu wa wilaya Moshi Chang'a akionekana kumgombeza Kaimu Mganga Mkuu wa Halmashauri ya wilaya ya Sumbawanga Dr. Eliana Yesaya hayuko (pichani) kutokana huduma mbovu zilizopo kwenye kituo cha wagonjwa wa Kipindupindu cha Muze.

Watu sita wamefariki dunia na wengine zaidi ya 100 wamelazwa na kuruhiwa kutokana na kuugua ugonjwa wakipindukipindu katika kata ya Muze wilayani Sumbawanga mkoani Rukwa.

Idadi hiyo inatokana na wagonjwa walioripoti kwenye kituo cha kipindupindu cha kata ya Muze killakini taarifa zaidi zimebainisha kuwa wapo watu wengine ambao wameugua na kufa katika kambi za wavuvi za ng’ambo ya Ziwa Rukwa na kufa pasipo kimyakimya pasipo serikali kuarifiwa.

Uchunguzi wa Mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa ugonjwa huo umelipuka kwa muda mrefu katika bonde la Ziwa Rukwa lakini umekuwa ukipungua na kurejea tena na kuongeza kasi yake katika kipindi cha mwezi Desemba mwaka jana baada ya kambi ya wavuvi ya kijiji cha Ilanga kukumbwa na tatizo hilo.

Hatahivyo tatizo hilo linaongeza katika kipindi hiki cha mvua kutokana na maeneo mengi katika bonde hilo la Ziwa Rukwa wakazi wake kutokuwa na vyoo huku baadhi ya Maafisa wa Afya wakituhumiwa kuchangia tatizo hilo kwa kueendekeza vitendo vya rushwa katika misako wanayoifanya kuwabaini wale wasio na vyoo.

“Zoezi la ujenzi wa vyoo kwenye maeneo ya kambi za wavuvi na vijiji jirani limekuwa gumu kwani kuna watu wamekuwa wakithubutu hata kuwapiga Mafisa Afya wanaokwenda kufanya ukaguzi kwenye maeneo hayo ya kambiu za wavuvi na mwisho wa siku wanaishia kumalizana kinyemela kwa kulipana fedha huku bado tatizo la kipindupindu likiendelea”. Alisema mmoja wa wakazi wa Muze ambaye hakutaka jinalake kutajwa.

Kufuatia hali hiyo juzi Kaimu Mkuu wa wilaya ya Sumbawanga, amabaye pia ni Mkuu wa wilaya ya Kalambo Moshi Chang’a alifanya ziara ya kushtukiza kwenye kambi ya kipindupindu ya Muze na kukuta wagonjwa wawili ambao wamelazwa kwenye kituo hicho wakiwa na hali mbaya , kutokana na uchafu na wagonjwa hao kukosa huduma muhimu huku Mkuu wa wilaya hiyo akigeuka mbogo kwa watoa huduma na Kaimu Mganga Mkuu wa halmashauri ya wilaya.

Mmmoja wa wagonjwa hao alikuwa amelazwa chini ya mti na kutundikiwa maji huku mwingine alikuwa amelazwa sakafuni ndani ya chumba kimoja kichafu na akiwa hajapatiwa huduma yoyote baada ya kituo hicho kukosa dawa na hata maji ya kuwatundikia wagonjwa hao hivyo kulazimika kununua wao wenyewe.

Kitendo hicho kilimkasirisha Mkuu huyo wa wilaya na kulazimika kupiga simu kwa Kaimu Mganga Mkuu wa Halmsahauri ya wilaya ya Sumbawanga Elina Yesaya akimtaka kueleza ni mkakati upi waliochukua katika kudhibiti kipindupindu kwa muda wote huo.

Chang’a alielezea kusikitishwa kwake na taarifa zilizotolewa wiki iliyopita kwenye kikao cha Ulinzi na Usalama cha wilaya ambapo ofisi ya Mganga Mkuu ilidai kuwa tatizo hilo limekwisha na hatua zimechukuliwa katika kuboresha kituo cha kipindupindu cha Muze ambacho Mkuu huyo wa wilaya alikikuta kikiwa kichafu na huku wahudumu wake wakikosa vifaa muhimu kama maji ya kutundikia wagonjwa na hata mopira ya kuvaa mikononi.

“Mganga kwanini unatesa hawa Watanzania, maana hapa nashuhudia wagonjwa wamejisaidia na hawajasafishwa, wamelazwa nje na mwingine kalazwa sakafuni, kituo kichafu na wewe upo !, ebu fikiria huyo angelikuwa mzazi wako halafu yupo kwenye hali hii ungejisikiaje, na umekaa ofisi pasipo kufika kuona tatizo, nakuagiza ndani ya saa sita uwe umeshafika hapa na huduma bora imepatikane, wala usinichokoze zaidi.” Alisema Chang’a wakati akizungumza na simu na Kaimu Mganga Mkuu.

Kwa upande wake Dkt. Yesaya alisema wamekuwa wakipeleka huduma zote kwenye kambi hiyo na wagonjwa wanahudumiwa vizuri na hatua zimechukuliwa kudhibiti kipindupindu kinyume na hali iliyokutwa na Mkuu wa wilaya hali iliyoonesha kuwa hakufika kwenye kituo hicho kujionea hali halisi.

Katika hatua nyingine Mbunge wa Jimbo la Kwela Ignas Malocha aliyeongozana na Mkuu wa wilaya kutembelea kituo hicho alilazimika kutoa fedha zake na kwenda kununua maji ya kutindikia wagonjwa hao baada ya kulazwa kwa muda mrefu kwenye kituo hicho wakiwa wamekosa huduma kutokana na kukosa uwezo wa kununua maji ya kuwatundikia.

Hatahivyo Chang’a aliaagiza kufungwa kwa muda wa wiki mbili migahawa yote kwenye mji nwa Muze huku akiagiza uongozi wa kata hiyo kufanya ukaguzi wa nyumba kwa nyumba na migahawa hiyo ili kubaini zileambazo hazina vyoo na kuwachukulia hatua kali za kisheria kwa wale watakaobainika kuwa hawana vyoo.


JIUNGE NA EDMO BLOG SASA

Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook,Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Edmo Blog Pekee!, kujiunga bonyeza hapa>>>Youtube

Tupe Maoni Yako lakini Usiandike Matusi



 
© Copyright EDMO BLOG | Designed By Peruzibongo