|
Na
Abdulaziz,Ruangwa
Wachimbaji
wadogowadogo wa madini
Wilayani Ruangwa pichani (kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya hiyo)
wametakiwa kuacha kufanya kazi katika mfumo usio rasmi badala yake
wabadilike
kwa kuingia katika mfumo rasmi ambao utawawezesha kukubalika na taasisi
za fedha
kutokana na kukua kwa sekta ya Madini Duniani ikiendana na Mabadiliko ya
Uchumi
hapa Nchini.
Wito huo Umetolewa
leo na Mkuu wa
Wilaya ya Ruangwa Mkoani Iindi,Bi Agness Hokororo alipokuwa
akifungua mafunzo ya siku mbili ya wachimbaji wadogo wa madini katika
wilayani
humo ambapo alibainisha kuwa uchimbaji mdogo ni sekta ya kibiashara
ambayo
inaweza kuongeza kipato cha wananchi kwa kuongeza ajira pamoja na
uchangia
ukuaji wa pato la taifa Licha ya kutokuwepo kwa taarifa sahihi za
uzalishaji na uuzaji wa madini na wachimbaji wadogo kutozifanya shughuli
za
uchimbaji madini kama shughuli maalum ambazo zinaweza kuajiri na
kuajiri
Mafunzo hayo ya
siku mbili
yamewezeshwa na Wizara ya Nishati na Madini na kuratibiwa na ofisi ya
Kamishna
wa Madini kanda ya kusini na kuhusisisha Wachimbaji
wadogo,Madiwani,Watendaji wa
vijiji/kata ambapo mada mbali mbali zitatolewa zikiwamao za Sheria ya
madini ya
mwaka 2010,Ufafanuzi wa sera ya madini,Fursa za madini zilizopo Ruangwa
na
Matumizi salama ya Baruti ambapo pia watapewa Mwongozo wa kuandaa mpango
wa
kutunza Mazingira(EPP0).
|